Jipatie MICHE BORA YA MATUNDA (Simu: 0763 071007)

Jipatie MICHE BORA YA MATUNDA (Simu: 0763 071007)

Jipatie Miche bora ya matunda mbalimbali kama Papai, Michungwa, Miembe, Miparachihchi, Pesheni (passion), Limao, Mipera, Michenza, Misatafeli, Topetope, Mifenesi minazi, n.k.

Embe
Miembe ni ile mifupi iliyofanyiwa Grafting. Miaka 3 tu unaanza kuvuna. Tofauti na ile mingine inayochukua miaka 7 kuanza kutoa matunda. Aina zilizopo ni Apple, Alfonso, Kenti, Red Indian, Apple, Bolibo, Dodo n.k Embe hizi ni zile za muda mfupi

Mwembe wa kisasa (Aina ya Apple). Hapa ndio umeenza kuzaa, ambapo ni mwaka wa 3 tu toka kupandwa. Mavuno huongezeka kadri mti unavyokuwa

Parachichi:
Miparachichi iliyopo ni ile ya muda mfupi na muda mrefu. Ya muda mfupi iliyopo ni HASS, hii ni chotara (hybrid) na inafaa sana kwa soko la nje. Wakulima wengi wanaolenga soko la ndani na nje wanapanda aina hii.

Parachichi aina ya HASS. Kwa sasa hizi ndio parachichi zenye soko zuri ndani na nje ya nchi.

Chungwa
Chungwa zilizopo ni zile zilizobebeshwa (Budding) ambazo huchukua miaka 3 tu kuanza kuvunwa
.

Papai
Miche ya Papai ipo ile mifupi. Miezi 6 hadi 7 unaanza kuvuna. Aina tulliynayo ni Malkia F1 (yenye rangi nyekundu ndani)
.

Migomba
Aina zilizopo ni: Mzuzu, Mtwike, Bukoba (Nshakara, Nyoya), Kisukari Mshale, Kimalindi nk

Pesheni
Aina zilizopo ni Yellow na Purple:
Aina ya Yellow au Njano: hizi ni zile pesheni za rangi ya njano, hufaa sana maeneo ya joto, na ni nzuri sana kwa juisi, maana sio chachu.
Aina ya Purple:, tunda lake ni la rangi ya zambarau na hufaa zaidi maeneo ya miinuko au sehemu zenye baridi.
Pesheni maeneo ya joto miezi 6 hadi 7 unaanza kuvuna, maeneo ya baridi huchukua miezi 9 hadi 10 kukomaa na kuanza kuvuna.

Kwa sasa tuna vitalu vya miche Dar (Ubungo Mawasiliano) na Morogoro mjini (SUA na Boma road).
Tunatuma pia popote ulipo ambako kunafikika na basi za kutokea Dar au Morogoro.

NB:Kwa wakazi wa Dar, tumeanzisha huduma ya ku deliver miche kwa mteja.. Ikiwa huna muda wa kufuata miche, sisi tunakuletea poppte ulipo (kisha unalipa pale unapofikishiwa miche yako).

Kwa mahitaji ya miche wasiliana nasi kwa simu 0763071007. Karibu sana.

Unaweza kujionea picha mbalimbali za miche hapa chini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *