Matumizi Ya Samadi (Samadi ya kuku, mbuzi na ng’ombe)

Matumizi Ya Samadi (Samadi ya kuku, mbuzi na ng’ombe)

Samadi ndiyo mbolea ya kwanza kuwekwa shambani bada ya kulima. Wakulima wengi hutumia mbolea ya samadi ya kuku kutegemeana na uwezekano wa kupatikana. Hata hivyo, samadi za mifugo tofauti zina virutubisho vyenye viwango vinavyotofautiana. Mkulima ni muhimu achague aina ya samadi ambayo inafaa zaidi katika mimea yake. Tofauti za samadi hizo ni hizi izfuatazo:

A) Samadi ya Kuku ina mbolea ya kukuzia (nitrojeni), Fosforasi na Potasium kwa wingi lakini ina uhaba wa mboji. Mbolea inayotokana na kinyesi cha kuku hufanya kazi haraka. Kiasi cha asilimia 70 ya nitrojeni iliyomo katika mbolea hii inaweza kutumiwa na mimea.

 B) Samadi ya ng’ombe ina asilimia kubwa ya mboji (78%) ikiwa ni pamoja na ambayo haiyeyuki haraka. Kwa hiyo samadi ya ng’ombe ni nzuri kwa kubadilisha hali ya udongo. Pamoja na kuwa mbolea kutoka zizi la ng’ombe ina Nitrojeni, Fosforasi na Potasium chache kuliko samadi ya kuku, inavyo virutubisho vingine vingi ambavyo vipo katika uwiano unaotakiwa na mmea.

Uwekaji wa samadi ya kukuzia unatakiwa ufanywe siku chache kabla ya kupanda au kupandikiza. Samadi inatakiwa ichanganywe na udongo vizuri na iwe na unyevu kwa siku chache za awali.

Kwa Ushauri wa Kitaalamu tucheki kupitia 0763071007

Kuhusu miche bora ya matunda: bonyeza hapa: https://kilimo.net/2019/04/22/miche-bora-ya-matunda-simu-0763-071007/

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *