Eliza: Mkulima wa Papai

Eliza: Mkulima wa Papai

Eliza: Mkulima wa Papai

Leo tunakwenda kumwangazia mkulima Eliza, mwandada mwenye dhamira ya kufanya makubwa kwenye kilimo.
Baada ya miezi kadhaa ya kufanya kazi na Eliza kwenye project yake ya Papai, sasa hivi Eliza ana furaha kama yote ??? akishuhduia namna project yake ilivyofanya vizuri.


Eliza ni mwanadada mpambanaji na tunajivunia sana kufanya naye kazi. Amelima Papai nusu ekari (Miche 400) maeneo ya Mlandizi, na tumekua naye toka hatua ya awali hadi sasa anapoanza kuvuna. Yuko makini sana kufuata ushauri wa kitaalamu tunaompatia mara kwa mara.

Malengo yake ni kuwa mzalishaji mkubwa wa Papai hapa Tanzania na kuwahamasisha Vijana wenzake (hususani Vijana wa kike) kujikita kwenye Kilimo. Sisi Kilimo biashara tuko bega kwa bega na Eliza kuhakikisha ndoto zake zinatimia.

Eliza alitutafuta mwaka jana mwezi July 2019, akiwa na lengo la kufanya kilimo cha Papai, ila akiwa hajui aanzie wapi. Eliza alisema kwamba alituona kwenye mtandao wa Youtube ambapo alitumiwa link na rafiki yake, akimwambia “hebu wajaribu hao”. Nakumbuka alikua na hofu kweli, maana pamoja na kwamba alikua na hamasa kubwa ya kufanya project ya papai, lakin pia alikua na hofu maana alikua akikatishwa tamaa na baadhi ya rafiki zake, akiambiwa kwamba kilimo cha papai ni kigumu sana.

Kilichokua kinampa hofu hasa ni kwamba kuna mmoja ya watu aliokua anawafahamu alinunua miche ya papai (kutoka kwa vishoka wa kilimo, hahahha) baadaye miche ile mingi ilikua madume (zaidi ya 50%) hivyo alipata hasara. Hivyo wakati Eliza anakuja kwetu ili kupata ushauri pamoja na miche, hofu hiyo ilikua dhahiri maana nakumbuka ilikua ngumu sana kumuaminisha kwamba sisi miche yetu ni Original, na yenye uhakika kwenye kuzaa. Baada ya majadiliano ya muda tulipanga appointment ya kwenda kutembelea baadhi ya mashamba ya wateja wetu ambao walishapata miche na ushauri kutoka kwetu. Baada ya siku mbili tulimpeleka Eliza kwenye shamba la mkulima wetu (Mr Amon) wa Chanika, baada ya kuona shamba lilivyopendeza na mipapai ilivyozaa alihamasika sana. Siku hiyo hiyo Eliza alithibitisha kwamba atapenda kufanya kazi na sisi. Hivyo siku chache baadaye tukaenda kumtembelea shambani kwake Mlandizi ambako amekodisha shamba karibu na mto Ruvu. Tulipofika shamba kiukweli, halikua shamba bali pori, hahahahha, maana palikua na nyasi kubwa na miti mingi ten yenye miiba. Hivyo kazi kubwa ilikua ni maandalizi, kuanzia kufyeka, kuong’a visiki na kulima. Tulitoa maelekezo namna shughuli hizo zinapaswa kufanyika na baada ya kama wiki kazi ya kusafisha shamba na kulima ikawa imekamilika. Tukafika tena shambani kwa ajili ya kutoa maelekezo na vipimo vya uchimbaji mashimo, na baada ya siku 3 kazi ikawa imekamilika, tukapeleka miche na kwenda kusimamia upandaji pamoja na kutoa mafunzo kwa msimamizi wa shamba. Tangu wakati huo tumekua tukimtembelea mara 1 hadi 2 kila mwezi kwa ajili ya kutoa ushauri wa kitaalamu pamoja na kutathmini maendeleo ya mradi.

Baada ya mafanikio kwenye mradi huu wa majaribio (pilot project) Eliza anatarajia kupanua mradi wake kufikia ekari 2 ndani ya mwaka huu 2020. Na ataendelea kuongeza mradi huu kila baada ya miezi 6 hadi 8.

Kwa leo tunaishia hapa, siku za usoni Tutaendele kukujuza zaidi.

Kwa ushauri kuhusu utaalamu wa kilimo cha Papai pamoja na miche tucheki kupitia 0763 071007
Pamoja na Miche utapatiwa ushauri wa kitaalamu kuanzia Upandaji hadi kuvuna.

When our customer is happy, we are super happy

#kilimobiashara

Response to "Eliza: Mkulima wa Papai"

  • Nimevutiwa sana na papai za sister Eliz anakaribia kutoka mimi ni muuguzi mwakani na staafu hoby yangu ni ilimo hivyo nitaomba ushauri wenu kwa sasa niko manyovu kigama nimelima papai miche kama miambili na hamsini lakini haina hali nzuri sijui ni kwa sababu ni ukada wa baridi naomba ushauri wenu 0754669130 napatikana kwenye whatsapp kwa namba hii na mtakia mafanikio mema binti Eliza afike mbali

    • Waoooh! Nimevutiwa sana na ujasiriamali wa dada eliza, but naomba kuuliza et! Parachichi inafaa kukuziwa na mbolea za chumvi chumvi?

  • Hongera sana Dada Eliza somo was mae wangu.Natamani sana kilimo hiki naomba msaada wako tafali. Mungu akubariki.

  • Nimesomea ualim sijapata ajira. Kwa sasa namifikiria nikasomee kilimo ili nijiajili katika kilimo. Naombeni ushauti chuo gani kinatoa mafunzo bora ya kilimo?

  • Napenda na Mimi kulima papai ninezoea kwamba mpapai unaoteshwa tu na kukua Bila maleeezi mengi kwa hio hii ya kisasa ninaona ni mradi wenye mambo meengi Sijui Kama nitaweza gharama ya kuwapata wataalam kila wakati…

  • MIMI Bw.Reuben Gurumo, mstaafu.nipo Bagamoyo MJINI.nimevutiwa na kilimo biashara Cha dada Eliza. MIMI Nina ninahitaji nianze kwa majaribio hapa hapa Bagamoyo MJINI nikifanikiwa nianze kwenye SHAMBA angalao eka 1 na kuendelea. Nina plots 2 sqm 1300 naishi hapa ukuni Bagamoyo ,KARIBU na mahakama ya wilaya ukuni, Bagamoyo Nina kisima Cha MAJI na water pump.kwa majaribio nahitaji ushauri nianze na Miche mingapi? Niihudumie vizuri kwani MUDA ninao na sehemu ya mazoezi

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *