Soko: Je utajuaje kipindi chenye soko zuri?

Soko: Je utajuaje kipindi chenye soko zuri?

Kama tulivyoshuhudia hivi karibuni namna bei ya nyanya na vitunguu ilivyopanda hadi kufikia kuwa gumzo kwa taifa zima. Mfano kuna maeneo tenga moja la nyanya la kilo 40 lilifika hadi 120,000 huku baadhi ya maeneo ya Dar, nyanya moja ikiuzwa hadi 500. Je ingekuaje kama wewe ndio ungekua unavuna wakati huo?

Je unajua ni kipindi gani kingine ambacho bei inakua nzuri hivi? Bahati mbaya wakulima wengi wakati wanapoona bei imepanda ndio hukimbilia kupanda nyanya wakidhani bei itaendelea kubaki juu, kwa mshangao mambo huwa tofauti sana na matarajio yao kwani kipindi wanapovuna wanakuta bei imeshaporomoka sana.
Je wajua kwamba kuna miezi sahihi ya kupanda ili uvune kipindi bei ya soko iko juu? Yaan unaweza kupangilia uzalishaji wako vizuri sana na ukawa na uhakika wa faida kila unapolima.

Wakaulima wengi wamekua wanakosea eneo hili sababu ya kukosa taarifa au kutokutafuta taarifa zinazohusiana na soko, kama vile kipindi chenye bei nzuri, ubora unaohitajika sokoni nk. Wengi hulima zao kwa kuangalia mazingira ya shambani(Msimu mzuri wa shambani) , yaani hali ya hewa, mvua nk bila kuhangaika kujua hali ya sokoni itakuaje pindi nitakapokua navuna. Kumbuka mazingira na hali ya hewa yanapofaa kwa kilimo, ujue ndio kipindi ambacho wakulima wengi wanaingia kulima na watavuna kwa pamoja, hivyo bidhaa husika itakua nyingi sokoni na hivyo kupelekea bei kuwa ndogo.

Kitu kingine ambacho wakulima hutumia kufanya maamuzi ya kuingia shambani, ni Bei/ soko zuri kwa wakati husika. Mfano hivi karibuni bei ya nyanya imepaa saana, kiasi kwamba wakulima wengi wametamani sana wangekua wanavuna nyanya wakati huo, Sasa na wengi wamehamasika wanaingia shambani wakidhani bei itazidi kupanda au itabaki juu mpaka watakapovuna nyanya zao, bila kujua kwamba wakaulima wengi nao wamewaza hivyohivyo na kuingia shambani kama wao, hii hupelekea wingi wa bidhaa sokoni, sababu wakulima wengi wanavuna kwa wakati mmoja na bei huporomoka (supply, demand and price).

Ikiwa unataka kufanya kilimo cha kibiashara, ni lazima uwe na uwezo au kiu ya kusaka taarifa na maarifa sahihi, na kuepuka kufuata mkumbo wa wakulima wengi. lazima ujitofautishe na wengine. Kufahamu kwa kina kuhusu haya na mengine ya muhimu nimekuandalia vitabu 3.

Napenda kukushirikisha OFA hii Maalumu kwa mwezi February 2020.

Nimeakuandalia vitabu 3 (Nyanya, Tikiti, na vitunguu) ambavyo vinatoa mafunzo kwa kina kuhusu kilimo cha Tikiti maji, Vitunguu maji na Nyanya.

Kupitia vitabu hivi utafahmu vyema kabisa miezi yenye bei nzuri na yenye bei mbovu, na nimekushauri hadi miezi ya kupanda ili kuvuna kipindi cha bei nzuri. Vilevile vikusaidia kufahamu mambo mengi sana ya shambani kama sifa za kuzingatia wakati wa kuchagua eneo zuri la kulima, namna ya kuchagua mbegu nzuri zenye kuzaa sana, namna ya kuongeza uzalishaji, kudhibti magonjwa na wadudu nk

Gharama hali ya Vitabu hivi ni 45,000 kwa vyote 3. Ila kwa mwezi huu wa February vitapatikana kwa punguzo kubwa la bei la 20,000, ambapo unapata vitabu vyote 3 badala ya bei yake halisi ya 45,000

Vitabu vilivyopo kwenye OFA hii ni:

  1. Mwongozo wa kilimo biashara cha Vitunguu maji
  2. Mwongozo wa Kilimo cha Tikiti maji
  3. Mwongozo wa Kilimo cha Nyanya

Vitabu hivi vinapatikana kwa mfumo wa nakala tete (softcopy) ambapo unatumiwa kwa njia ya mtandao (email, au Whatsapp).
Unafanya malipo ya 20,000 Kwa mpesa Tigo pesa 0712578307 (jina litaonyesha Daudi Mwakalinga)
Ukishafanya malipo unatuma Ujumbe wenye Jina na email yako kwenda 0763 071007 au 0712 578307.

VItabu utavipata ndani ya dakika 5 hadi 10 baada ya kufanya malipo.

NB:
Ukimaliza kusoma vitabu hivi, alafu ukakuta hakuna jipya ulilojifunza, tunakurejeshea fedha yako (If you find what we teach in these books is not new to you we refund your money.. period)

OFA hii ni maalumu kwa mwezi huu February, na itaisha 29 February 2020 saa 12:00 jioni.

Kwa ushauri wowote kuhusu kilimo wasiliana nasi:

Simu: 0763 071007

EMail: ushauri@kilimo.net

Response to "Soko: Je utajuaje kipindi chenye soko zuri?"

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *