Greenhouse Mpya – Dege Kigamboni

Greenhouse Mpya – Dege Kigamboni

Greenhouse Mpya – Dege Kigamboni

Project ya Greenhouse hapa Dege, Kigamboni Dar, inaendelea vyema. Leo tumekamilisha zoezi la kufunika. Tunaelekea ukingoni kabisa kukamilisha ujenzi wa project hii.

Greenhouse hii ni ndogo na imejengwa nyumbani kabisa (home compound)

Greenhouse hii itakua maalumu kwa ajili ya kulima Pilipili Hoho za rangi  pamoja na Nyanya.

Pilipili Hoho za rangi (nyekundu na njano) ndizo zitakazoanza kupandwa (kuanzia mwezi huu March), ili kulenga soko zuri la kuanzia mwezi May hadi August/ September)- Kipindi hicho hoho za rangi bei yake huwa nzuri sana na hufika hadi 4,000 kwa kilo. Hoho zitakazopandwa ni zile za kuvuna kwa muda mrefu (ambazo unaweza kuvuna kwa zaidi ya miezi 6 tokea mvuno wa kwanza)

Nyanya, zitapandwa kuanzia October/November hii itapelekea uvunaji wa nyanya kuanza January hivyo kukutana na soko zuri la nyanya ambalo hutokea kuanzia  kipindi cha mwezi January hadi April/May

Greenhouse hii ni ya mteja wetu Madam WinFrida ambaye ni mwajiriwa. Ndoto ya WInfrida ni kuwa mkulima mkubwa wa kilimo cha kisasa, kwa kuzalisha mazao ya mbogamboga na matunda kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Lengo lake pia ni kuachana na kuajiriwa na kujikita zaidi kwenye Kilimo hichi.


Tutaendelea kukulete maendeleo ya Greenhouse hii pamoja na nyingine tunazozijenga na tutakazozijenga.

Pia nikukumbushe kwamba OFA yetu ya Greenhouse bado ipo, ila zimebaki nafasi 3 tu za OFA hii, 

Tucheki kupitia 0763 071007

Kwa maelezo zaidi kuhusu OFA yetu hii unaweza kupata maelezo zaidi hapa chini:

Kwa mwezi huu wa March 2020  tunatoa OFA ya Punguzo la ufungaji wa Greenhouse. OFA inajumuisha vitu hivi:

  1. Punguzo la gharama ya greenhouse.  Punguzo la bei litakua kuanzia 10%  hadi 30% kutegemeana na ukubwa wa greenhouse 
  2. Ongezeko la vifaa au huduma, mfano tank la maji. Awali tank la maji ilikua ni juu ya mteja, ila kwenye Ofa hii,  mteja atapatiwa Tank la maji bure kabisa. Tank la Maji kuanzia lita 500,1000, 2000 n.k Ukubwa wa tank la maji utategemeana na ukubwa wa greenhouse. 
  3. Mbolea na madawa ya kuanzia
  4. Soko. Kuunganishwa na masoko
  5. Hakuna gharama za usafiri. Awali mteja alikua anachangia gharama za kusafirisha materials mpaka Site anakotaka kufunga greenhouse. Kwenye OFA hii mteja hatachangia gharama za usafiri.

Hizo ni baadhi  tu ya OFA zitakazotolewa, Maalum kwa mwezi March 2020

Ukubwa wa Greenhouse na bei zake za OFA:

Mita 6 kwa 12 – milioni 4.5 (badala ya 5m)
Mita 8 kwa 15 –  Milioni 5 (badala ya 6M)
Mita 6 kwa 24 Milioni 6.5 (Badala ya 7.2M)
Mita 8 kwa 30 Milioni 9 (Badala ya 12)
Mita 16 kwa 30 -Milioni 16 (Badala ya 18M)

NB: Tutakufungia Ukubwa wowote unaotaka kulingana na bajeti yako

OFA hii pia itaambatana na Package ya vitu vifuatavyo:

Upimaji wa udongo. Kupimiwa udongo wa eneo ambalo GH inajengwa, ili kujua sifa za udongo na virutubisho vilivyomo. Hii itasaidia pia kujua aina za mbolea zitakazotumika.
Kufungiwa vifaa vya umwagiliaji matone (drip irrigation)

Tenki la maji. Utafungiwa tank la Maji kuanzia lita 1000, 2000, 5000 n.k kutokana na ukubwa wa Greenhouse

Mbegu/Miche. Utapatiwa mbegu au miche ya zao unalotaka kulima

Mbolea na madawa: utapatiwa mbolea na madawa yote muhimu  ya kuanzia- mbolea na dawa zitakazotolewa zitatosha kwa miezi 2 hadi 3 ya mwanzo. 
Kufungiwa crop support– hizi zinasaidia kushikilia mazao kwenye Greenhouse

Upandaji. Tunakusaidia kupanda miche/mbegu za zao tulilokubaliana. -Unakabidhiwa greenhouse/ikiwa imekamilika kila kitu, kazi yako ni kuanza kuhudumia tu.

Mafunzo. Tunatoa mafunzo (training) ya usimamizi wa Greenhouse kwa mfanyakazi wako ambaye atakua anahudumia Greenhouse. Mafunzo haya yatafanyika kwa muda wa miezi 2 hadi 3.
Kutembelewa na Kupewa ushauri wa mara kwa mara

Masoko. Tunatoa usaidizi katika kutafuta na kuunganishwa na soko la uhakika.


Tutakufuata popote pale ulipo Tanzania

NB: OFA hii ni maalumu kwa mwezi March 2020.
Simu: 0763 071007
email: ushauri@kilimo.net

Response to "Greenhouse Mpya – Dege Kigamboni"

  • Habari za kazi,Am interested with your services and offer,nilitaka kufahamu izi ofa huwa kipindi gani nijaribu kuchukua iyo ya mita 6 kwa 24mita ambayo ni 6.5milioni?

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *