FAIDA ZA KUUNGANISHA/KUBEBESHA MICHE (Grafting/budding)

FAIDA ZA KUUNGANISHA/KUBEBESHA MICHE (Grafting/budding)

Sehemu mbili za mimea ya jamii moja (muembe kwa muembe, mparachichi kwa mparachichi) au miche ya aina tofauti kidogo ila jamii moja (mchungwa kwa mlimao) ndiyo inayoweza kuunganishwa au kubebeshwa. Hii kwa kitaalamu huitwa Grafting au Budding. Teknolojia hii ya ubebeshaji wa mimea husababisha upatikanaji wa matunda yenye sifa ambazo wakulima wanazihitaji kwa mfano ladha nzuri, ukubwa wa matunda na ubora unaokidhi soko.

Grafting/Budding Hii huusisha sehemu muhimu mbili:

(a) Sehemu ya shina (mche shina) ambayo hutokana na kuotesha mbegu za mmea ulichaguliwa kuwa mmea shina.

(b) Sehemu ya tawi (kikonyo) huchukuliwa kutoka mti mama wenye sifa za kuzaa matunda mengi na yaliyo bora, ambayo ndiyo yanayotakiwa kama zao.

Mche uliyounganishwa kwa kutumia kikonyo au kitawi kilichochukuliwa kutoka kwa mche mama uliokwisha zaa, utazaa matunda mapema. Kwa mfano, miche ya miembe na michungwa na jamii yake huzaaa baada ya miaka 3-4 hivi ukilinganisha na miaka 7-8 kama miche itapandwa moja kwa moja kutokana na mbegu bila kuunganishwa.

Mche uliounganishwa unadumisha/endeleza sifa halisi ya mmea mama ambao kikonyo chake kimetumika kwenye kuunganisha.

Kuunganisha mche kunatoa nafasi ya kutumia mimea shina ambayo inauwezo kwa mfano wa kuvumilia ukame, magonjwa na ama hali ya udongo ambayo mmea tawi usingeweza kuvumilia

Mti wa mwembe uliofanyiwa Grafting.

Mimea inaweza kuunganishwa kwa sababu mbalimbali zingine. Kwa mfano kuna aina ya mimea ambayo haina uwezo wa kutoa mbegu (ndimu zisizo na mbegu, machungwa yasiyo na mbegu). Miche inaweza kuunganishwa kwa sababu za kudhibiti magonjwa au wadudu, Pia miti iliyounganishwa itakuwa na umbile dogo endapo mmea shina una asili ya kuwa na umbile dogo.

Kuna njia kuu mbili zinazoweza kutumika katika kuunganisha miche. Njia hizi zimegawanya kufuatana na aina ya kikonyo kinachotumika katika uunganishaji.

 • Kuunganisha kwa kutumia kijicho (budding) – Hii hufanyika kwa mimea jamii ya chungwa, limao ndimu nk

• Kuunganisha kwa kutumia kitawi / kikonyo (grafting)- Hii hufanyika kwa mimea kama miembe, parachichi.nk

Jipatie miche bora ya Matunda mbali mbali iliyofanyiwa Grafting au Budding kama Miembe, parachichi, Mikorosho, Michungwa, Milimau, Michenza nk. Pia tunayo miche ya papai za kisasa zile zenye ranfi nyekundu ndani (Malkia F1)

Pamoja na Miche utapatiwa ushauri wa kitaalamu.

Vitalu vyetu vya miche vinapatikana Dar na Morogoro. Kwa Dar, tupo hapa Ubungo Mawasiliano., Mlimani City na Mabwepande. Pia tunafanya delivery, kwa wakazi wa Dar, (kuanzia miche 50 tunakuletea kwa gharama nafuu kabisa). Kwa wateja wa mikoani tunatuma, na miche inafika salama kabisa.
Mawasiliano: Simu 0763 071007
Email: ushauri@kilimo.net
Website: www.kilimo.net

Response to "FAIDA ZA KUUNGANISHA/KUBEBESHA MICHE (Grafting/budding)"

  • Ahsante sana ndugu Daudi nazidkunufaika sana kwamasomo yakńa mm najiandaakuanza kulima nimevutiwa nauwekezaji huu wakilimo

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *