Aina za machungwa zinazozalishwa nchini Tanzania

Aina za machungwa zinazozalishwa nchini Tanzania

Kuna aina nyingi sana za machungwa zinazozalishwa kote dunia. Hizi ni baadhi ya aina za machungwa yanayozalishwa nchini Tanzania.

1. Late Valencia: Aina hii ya machungwa huchelewa kukomaa hivyo kumpa mkulima nafasi ya kupanga bei sokoni. Pia, aina hii hustahimili shurba za usafiri wakati wa kupeleka sokoni. Ina maji mengi, tamu na sukari ya kutosha.

2. Early Valencia: Aina hii huwahi kukomaa. Aina hii humuwezesha mkulima kupata kipato mapema. Haitoi nafasi kwa mkulima kusubiria kupata bei nzuri kwani huharibika haraka. Ni tamu na ina sukari nyingi.

3. Delta Valencia: Hii ni moja ya aina nzuri sana ya chungwa. Aina hii haina mbegu ndani ya tunda. Inafaa na kutumiwa sana na wasindikaji wa juisi. Ni tamu na ina sukari nyingi.

4. Jaffa: Hii ni aina iliyozoeleka sana kwa wazalishaji wa machungwa hasa mkoani Tanga. Aina hii huzaa kuliko aina zote na ni kubwa. Yana maji mengi, hukomaa mapema. Hayastahimili kukaa shambani muda mrefu baada ya kuiva, na pia haistahimili misukosuko ya usafirishaji.

5. Washington navel: Hii ni aina ya chungwa ambayo haina mbegu ndani yake. Ni moja ya machungwa yanayopendwa sana na walaji. Aina hii huharibika kwa urahisi endapo haitasafirishwa kwa uangalifu kwenda sokoni.

6. Mediterranean sweet: Aina hii huzaa vizuri sana. Ina maji mengi na ni tamu sana. Huwai kukomaa.

7. Pineapple: Hii ni aina ya chungwa ambayo imepewa jina hilo kutokana na ladha yake kufanana na ya nanasi. Aina hii ya chungwa huwahi sana kukomaa na ni nyepesi kuharibika.

8. Chenza: Hii ni moja kati ya jamii za chungwa. Aina hii hukomaa haraka. Likishakomaa linahitaji kuvunwa kwa haraka. Lina umbile dogo, maganda yake ni laini, hivyo halistahimili shurba kwa muda mrefu

Matumizi ya machungwa

 • Machungwa hutumika kwa kuliwa kama tunda.
 • Hutumika kwa kutengenezea viburudisho kama vile juisi.
 • Maganda ya matunda hutumika kwa kusagwa na kutengenezea dawa.
 • Unga unaotokana na maganda ya machungwa hutumika kama kiuongo cha kuongeza harufu na ladha kwenye vitafunwa.
 • Machungwa hutumika kama lishe ya mifugo

Faida za uzalishaji wa machungwa

 • Miti ya machungwa hutumika kama njia moja wapo ya kuhifadhi mazingira.
 • Ni njia moja wapo ya kipato kwa mkulima.
 • Machungwa ni chanzo kizuri cha lishe kwa familia

Karibu ujipatie Miche bora ya matunda. Tunayo miche ya Papai, Miembe,  Michungwa,  ndimu,  parachichi,  Migomba  nk

Pamoja na Miche utapatiwa ushauri wa kitaalamu kuanzia Upandaji,  utunzaji hadi Mavuno.

Tunafanya delivery, kwa wakazi wa Dar, (kuanzia miche 50 tunakuletea kwa gharama nafuu kabisa). Kwa wateja wa mikoani tunatuma, na miche inafika salama kabisa.

Mawasiliano: Simu 0763 071007

Email: ushauri@kilimo.net

Website: www.kilimo.net

Response to "Aina za machungwa zinazozalishwa nchini Tanzania"

 • Leave a Reply

  Your email address will not be published. Required fields are marked *