Faida za Greenhouse

Faida za Greenhouse

Greenhouse(Banda Kitalu):ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu.Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa. Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.

Zifuatazo ni baadhi tu ya Faida za Greenhouse

  1. Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi, ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.
  2. Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya uharibifu wa mazao.
  3. Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
  4. Uwezo wa kupata soko zuri la mazao. Greenhouse itakuwezesha kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu,ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei nzuri
  5. Ufanisi katika utumaji wa dawa (viwatilifu) katika kudhibiti wadudu na magonjwa.
  6. Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti wake ni rahisi. Miundombinu ya umwagiliaji inayotumika hapa ni umwagiliaji wa matone (drip irrigation) ambapo maji yanakwenda pale penye mmea tu.
  7. Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili ya kuzoea mazingira ya nje kwanza.
  8. Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (soilless culture).Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuziwa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea

OFA OFA OFA; Jipatie Greenhouse za bei nafuu.
Kwa Mwezi January na February, tunakuletea OFA maalumu ya kutengenezewa Greenhouse kwa gharama nafuu


Ukubwa wa Greenhouse na bei zake:
Mita 6 kwa 24 Milioni 6.5M
Mita 8 kwa 15 Milioni 5.5
Mita 8 kwa 30 Milioni 10.5
Mita 16 kwa 30 -Milioni 18.5

NB: Tutakufungia Ukubwa wowote unaotaka kulingana na bajeti yako

OFA hii pia itaambatana na Package ya vitu vifuatavyo:

  1. Upimaji wa udongo. Kupimiwa udongo wa eneo ambalo GH inajengwa, ili kujua sifa za udongo na virutubisho vilivyomo. Hii itasaidia pia kujua aina za mbolea zitakazotumika.
  2. Kufungiwa vifaa vya umwagiliaji matone (drip irrigation)
  3. Tenki la maji. Utafungiwa tank la Maji kuanzia lita 1000, 2000, 5000 n.k kutokana na ukubwa wa Greenhouse
  4. Mbegu/Miche. Utapatiwa mbegu au miche ya zao unalotaka kulima
  5. Kufungiwa crop support- hizi zinasaidia kushikilia mazao kwenye Greenhouse
  6. Upandaji. Tunakusaidia kupanda miche/mbegu za zao tulilokubaliana.
  7. Unakabidhiwa greenhouse/ikiwa imekamilika kila kitu, kazi yako ni kuanza kuhudumia tu.
  8. Mafunzo. Tunatoa mafunzo (training) ya usimamizi wa Greenhouse kwa mfanyakazi wako ambaye atakua anahudumia Greenhouse. Mafunzo haya yatafanyika kwa muda wa miezi 2 hadi 3.
  9. Masoko. Tunatoa usaidizi katika kutafuta na kuunganishwa na soko la uhakika.

NB: OFA hii ni maalumu kwa Mwezi January na February 2020.

Tutakufuata popote pale ulipo Tanzania
Simu: 0763 071007
email: ushauri@kilimo.net

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *