Mwongozo wa Kilimo Bora cha Papai

Mwongozo wa Kilimo Bora cha Papai

Utangulizi:
Mapapai ni zao moja kati ya mazao ya matunda yenye vitamini A na madini ya kalsiamu kwa wingi. Inaamanika asili ya papai, ni huko nchi za Amerka ya kati, (Mexico), ndipo zao ili likasambaa duniani kote. Kwa sasa zao hili hulimwa karibu kila mahali hapa nchini. Papai ni moja ya mazao yenye faida kubwa na yenye soko la uhakika.

Aina za Mbegu
Kuna aina 3 za mbegu za papai.

1. Mbegu za kienyeji (local varieties). hizi ni aina ya papai za kienyeji ambazo, mara nyingi hazifahamiki majina yake. Mbegu zake huwezi zipata kwenye mfumo rasmi wa mbegu (madukani) nk. mara nyingi mbegu hizi hupatikana kwa kuchukua matunda yaliyoiva na kuchukua mbegu zake.. kiswahili cha mtaani husema mbegu za kukamua..


2. Aina za kawaida (open pollinated varieties kwa kifupi OPV). Mfano wake ni kama Calina nk hizi hua na uzao wa kati.


3. Chotara (hybrid). Mfano Malkia F1, Sinta F1, Red royal mk. Hizi hufanya vizuri maeneo mengi.. hua na uzao mkubwa kuliko aina nyingine tulizojifunza hapo juu


MAMBO YA KUZINGATIA WAK ATI WA UZALISHAJI
Ili kupata mazao yenye ubora unaotakiwa ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo bora za uzalishaji
wa mapapai. Ubora wa matunda baada ya kuvunwa hutegemea jinsi yalivyozalishwa. Baadhi
ya kanuni hizo ni kama zifuatazo:
Kuchagua aina bora
Chagua aina bora ya kupanda kulingana na mahitaji ya soko.
Kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu
Mapapi hushambuliwa kwa urahisi na magonjwa na wadudu, hivyo ni muhimu kufanya ukaguzi
wa mara kwa mara ili kugundua dalili za mashambulizi.
Endapo kuna dalili za mashambulizi, dhibiti mapema ili kuzalisha mazao bora yanayoweza
kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Pia hakikisha shamba na barabara zake ni safi wakati wote ili kurahisisha uvunaji na
usafirishaji.

Maandalizi kabla ya kuvuna
Kukagua shamba
Kagua shamba kuona kama kuna mapapai yaliyokomaa
Mapapai hukomaa katika kipindi cha miezi minne hadi mitano kutoka maua yanapochanua.


Dalili za mapapai yaliyokomaa
Tunda hubadilika rangi kutoka kijani kibichi na kuwa ya kijani nyepesi hadi manjano.

Kuvuna
Uvunaji bora wa mapapai ni wa kutumia mikono ambapo tunda huchumwa kwa mkono au kwa kutumia vichumio maalumu.
Vuna mapapai yaliyokomaa tu
Vuna mapapai pamoja na vikonyo vyake
Vuna kwa uangalifu ili kuepuka kudondosha matunda
Matunda yakidondoka, huchubuka, hupasuka au hupondeka hivyo husababisha upotevu.
W eka mapapai kivulini mara baada ya kuvuna
Kuchambua, Kusafisha na Kupanga Madaraja
Ni muhimu kuchambua mapapai ili kutenga yaliyooza, kupasuka na yenye dalili za magonjwa au kubonyea. Lengo la kuchambua ni kupata matunda yenye ubora kulingana na matumizi , kwa mfano kusindika, kuuza au kusafirisha.
Matunda yaliyooza na yenye wadudu ni vyema yafukiwe ili kuangamiza wadudu waharibifu
na vimelea vya magonjwa, na pia kuzuia kuenea kwa wadudu na magonjwa hayo.
Matunda yaliyopasuka, kubonyea au kuchubuka kidogo yatumike haraka kwa kuliwa.
Matunda mazuri ambayo hayajapata madhara yoyote yatumike kwa ajili ya kusindika, kuliwa, kuuzwa au kusafirishwa.


Mwongozo wa Kulima Papai (Master Plan)
Tumekuandalia Mwongozo (Master plan) wa Kilimo hichi, utakaokuongoza hatua kwa kwa hatua kuanzia namna ya kuandaa shamba, kuchimba mashimo, upandaji kwa kutumia miche bora, kudhibiti magonjwa na wadudu kwa kupiga dawa, kuweka mbolea, kumwagilia na mengi mengi.
Hapa chini nimekupa kionjo tu cha baadhi ya mambo utakayoyakuta kwenye Master Plan ya kilimo cha Papai.


Baadhi ya Yaliyomo kwenye Mwongozo (Master Plan):
Uandaaji wa mashimo kitaalamu, na namna ya kutengeneza mchanganyiko mzuri wa udongo, mbolea, majani makavu na majivu.
Programu ya upigaji dawa za magonjwa na wadudukuanzia mwanzo hadi mwisho. Hapa tumependekeza dawa zenye ufanisi mzuri kwenye kudhibiti magonjwa na wadudu wasumbu kwenye mipapai.  Wale wadudu weupe wasumbufu, ambao huweka utandao mweupe (Kitaalamu huitwa White mealybug), tumeweka dawa nzuri yenye kuwamaliza kabisa. Hivyohivyo kwa magonjwa na waududu wengine Muongozo huu unapendekeza dawa  zake na namna ya kuzipiga
Programu ya Uwekaji Mbolea:kuanzia mbolea ya kupandia hadi mbolea za kuimarisha matunda kua na ngozi imara. Wakati gani wa kuweka mbolea hizo, na  kiwango cha kuweka kwa mmea. Pia utajua namna ya kuchanganya mbolea mbili kwa uwiano mzuri wenye kuleta matokeo mazuri.
Programu ya Mbolea za majani (Booster):hapa utazifahamu mbolea zote za majani kuanzia za wakati mimea ni midogo hadi zile za kipindi cha matunda. Ili kuleta ufanisi zaidi tumeonyesha namna ya kuchanganya mbolea hizi za majani (boosters) na dawa za wadudu
Programu ya Umwagiliaji:Hapa utafahamu kiwango cha maji kinachohitajika kwenye kila hatua ya ukuaji ya mipapai. Pia utafahmu ni wakati gani wa kumwagilia kila siku, kila wiki na ratiba ya mwezi.
Shughuli nyingine zote muhimu zipo, na zimewkwa kwa mtiririko mzuri ambao kila mkulima ataelewa na kuweza kutekeleza ipasavyo.
Kwa wakulima watakaotumia Master Plan watapewa fursa ya kupata mafunzo na ushauri wa mara kwa mara  kwa msimu mzima wa kwanza: (ushauri na mafunzo haya kuhsiana na papai yatatolewa bure kwa wale watakatumia huduma yetu hii ya Master plan)


Gharama ya Muongozo (Master Plan)
Kwa sasa Mwongozo huo unapatikana kwa bei ya OFA ya 20,000 tu. Pia OFA hiyo itaambatana na kupatiwa Mchanganuo wa Gharama na FAIDA (Cost Benefit Analysis au CBA) kwa zao la Papai. Mchanganuo huu umeorodhesha vitu vyote vinavyohitajika pamoja nagharama zake, Vilevile umekusaidia kukokotoa Faida inayopatikana ukilima papai ekari 1.

Yaani ukilipa hiyo 20,000 unapatiwa Master Plan pamoja na CBA kama bonus.  Baada ya muda wa ofa kuisha Muongozo huu utapatikana kwa gharama ya 50,000. Usikubali kupitwa na OFA hii,
Namna ya Kupata nakala yako ya Mwongozo:
Unafanya malipo ya 20,000 Kwa mpesa 0763 071007 au Tigo pesa 0712578307 (Jina Litaonyesha Daudi Mwakalinga)
Ukishafanya malipo unatuma Ujumbe wenye Jina na email yako kwenda 0763 071007 au 0712 578307. Kama huna email na ungependa kutumiwa Kitabu kwa Whatsapp au Telegram basi utatuma ujumbe WhatsApp au Telgram kwenda namba 0763 071007
Karibu sana
Daudi Mwakalinga
0763 071007
Email: ushauri@kilimo.net

Response to "Mwongozo wa Kilimo Bora cha Papai"

  • ahsante mwakalinga tumekusoma vizuri,nitatumia nafasi hii ya ofa kupata mwongozo.
    kwa sasa niko shinyanga sijui wewe uko mkoa gani,pia suala la kupima udongo ni vipi kilmo cha papai?

  • Napenda jua kuna master plan za mazao yepi apart from papai na upatikanaji wake upoje na kama zipo za mifugo taarifa pia ntapenda pata

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *