Faida za Miparachichi, Miembe na Michungwa

Faida za Miparachichi, Miembe na Michungwa

1.1 MIPARACHICHI

 • Miparachichi imekuwepo nchini kwa miaka mingi. Katika mikoa ya kaskazini (Kilimanjaro na Arusha) pamoja na kutumika kama matunda, maparachichi yalibeba jina la chakula cha mbwa kwa kuwa mara nyingi yalipodondoka kutoka kwenye miti yaliliwa na mbwa. Hata hivyo, mikoa ya kusini (Mbeya) maparachichi
  yamekuwa tunda muhimu katika milo yote.
 • Utafiti umeonesha kwamba maparachichi yana mafuta muhimu yanayoondoa mafuta yanayoganda kwenye mishipa ya damu. Pia yana virutubisho vinavyofanya damu itembee kwa urahisi mwilini. Maparachichi yana virutubisho vya vitamini E. Kwa sababu hii maparachichiyanatumika katika kutengeneza vipodozi ya ngozi na nywele.
 • Matunda ya parachichi yanaweza kuliwa kwa namna tofauti. Yanaweza kuliwa kama kituliza njaa wakati ukisubiri chakula kingine au kilainisha chakula baada ya mlo. Pia parachichi linaweza kuliwa sambamba na chakula kingine kwa mfano ndizi za kuchoma. Maparachichi yanatumika pia kutengeneza juisi.
 • Matunda machanga yaliyoanguka yanatumika kuharakisha uivishaji wa ndizi kwa kuzifanya ndizi ziive zote kwa pamoja.
 • Majani ya miparachichi yanatumika kulishia mifugo kama mbuzi na ngombe wakati miti yake inatoa mbao nzuri za kutengenezea samani.
 • Hivyo miparachichi inaweza kuwa chanzo kizuri cha pesa kwa familia na wajasiliamali soko lake
  likiboreshwa.
 • Miparachichi huweza kustawi sehemu nyingi zenye hali ya hewa ya kitropiki iliyo na kipindi cha ubaridi, joto kiasi na mvua za kutosha.
 • Hivyo, hapa nchini kilimo chake kimeshamiri zaidi kwenye maeneo ya nyanda za juu mikoa ya Mbeya, Iringa, Morogoro, Kilimajaro na Arusha. Sehemu nyingine zilizo kwenye miinuko mfano Lushoto mkoani
 • Tanga zao hili laweza kulimwa. Hata hivyo kulingana na aina ya miparachichi, maeneo ya nyanda za chini yasiyo na vipindi virefu vya ukame yanaweza pia kustawisha zao hili. Kwa vile miparachi ni miti inayo kua haraka na haipukutishi majani, hivyo ni mti mzuri katika kuhifadhi mazingira.
 • Endapo miti hii itapandwa kwa wingi itakuwa ni kivuto cha ukusanyaji wa hewa ya ukaa inayotokana na ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi.

1.2 MIEMBE

 • Embe ni tunda maarufu na limekuwa likitambulika kama mfalme wa matunda. Matunda ya embe yanatumika yakiwa mabichi au yameiva. Matunda yaliyoiva yanaliwa kama tunda au pia yanaweza kutengenezwa juisi na jam.
 • Embe mbichi hutumika katika kutengeneza achali. Kama ilivyo kwa miparachichi, miembe hukua haraka na haipukutishi majani na hivyo ni mti unaobadilisha mazingira ya mashamba na kuleta hali ya ukijani kwa
  mwaka mzima.
 • Miti ya miembe ikipandwa kwa mpango mzuri mashambani inasaidia kurekebisha hali ya hewa kwa kupunguza joto, kuvuta mawingu ya mvua, kupunguza kasi ya upepo, kupunguza mmomonyoko wa ardhi na kufyonza hewa ya ukaa.
 • Hivyo Miembe nayo ni miti mizuri kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
 • Miti hii ikipandwa mashambani kwa mpangilio mzuri wakulima wataweza kulima mazao menginena hivyo kujipatia fedha zaidi, matunda na hata kuni.
 • Miembe hustawi sehemu zenye joto la wastani na lenye maji au mvua za kutosha, hata hivyo miembe haistawi vizuri katika maeneo yenye baridi kali na mvua nyingi kwa mwaka kwa kuwa inahitaji kipindi cha ukame cha miezi isiyopungua miwili hadi mitatu ili kuwezesha kutoa maua. Pia miembe hihutaji udongo wenye kina usio twamisha maji na usio na chumvi chumvi.

1.3 MICHUNGWA

 • Michungwa pamoja na aina ya matunda yaliyo kwenye jamii yake kama vile machenza, madaransi, mapomelo, malimau, ndimu n.k. pia ni matunda maarufu katika sehemu za nchi za joto na zile za joto kiasi.
 • Matunda haya hutumika mara nyingi yakiwa yameiva kwa kuyala moja kwa moja au kutengeneza juisi na jam.
 • Yana vitamini C nyingi pamoja virutubisho vingine vinavyohitajika kwa mwanadamu.
 • Machungwa pamoja na jamii yake huwapa wakulima faida wakati wa mauzo na pia huongeza thamani ya mashamba yao. Wadau wengi hunufaika kutokana na kilimo cha matunda haya. Kwa mfano walanguzi na wafanya biashara wengine kama wale wasafirishaji hujipatia faida.
 • Miti ya michungwa kama ilivyo kwa miti mingine, kutumia hewa ya ukaa na hutengeneza kivuli na hivyo kupoza joto.
 • Michungwa huweza kustawi kutoka ukanda wa pwani hadi sehemu za miinuko ya kiasi cha mita 2000 kutoka usawa wa bahari. Pia miembe hihutaji udongo wenye kina usio twamisha maji na usio na chumvi chumvi.
 • Machungwa pia huhitaji kipindi kifupi cha ukame ambapo baada ya kupata maji hutoa maua.

OFA! OFA! OFA!
Ni Ofa ya miche ya papai, miembe, miparachichi, michungwa, mipesheni, Mipera, limao, michenza, migomba nk
Sasa unaweza kupata miche bora ya matunda kwa bei ya punguzo:
Papai fupi (Malkia F1), ofa ni: 4,000 kwa mche badala ya 5,000
Miembe, Michenza, Migomba, Parachichi na Michungwa ofa ni: 3,000 kwa mche badala ya 3,5000
Mipera, mipesheni ofa ni: 2,000 kwa mche badala ya 2,500
OFA hii mwisho ni 15 May 2018.
Tunakutumia miche popote ulipo Tanzania. Karibu sana ujipatie miche bora na ya kisasa.
Mawasiliano: Simu 0763 071007
Email: ushauri@kilimo.net 


Response to "Faida za Miparachichi, Miembe na Michungwa"

 • Leave a Reply

  Your email address will not be published. Required fields are marked *