Fursa ya kuwa wakala/muuzaji wa Vitabu vya kilimo biashara

Fursa ya kuwa wakala/muuzaji wa Vitabu vya kilimo biashara

TImu ya kilimo.net inatangaza fursa za kuwa wakala/muuzaji wa vitabu vya kilimo biashara vinavyotolewa na timu ya wataalamu wetu.
Sifa zifuatazo zinahitajika:

 • Lazima awe mwaminifu sana tena sana. Hiki ndio kigezo kikuu.
 • Awe tayari kufanya kazi kwa commission. Malipo yake yatatokana na mauzo anayofanya kulingana na makubaliano.
 • Awe tayari kufanya kazi kwa bidii sana
 • Awe na uwezo wa kushawishi na awe mchangamfu na aliyehamasika
 • Awe na ujuzi wa kuuza moja kwa moja kwa wateja (direct selling)
 • Awe mbunifu sana katika kazi yake
 • Awe na umri wa miaka kati ya 20 hadi 30.
 • Awe na uwezo wa kusoma na kuandika
 • Awe mtu wa kupata matokeo sio mtu wa kutoa visingizio
 • Awe mtu wa kufikiria suluhisho na sio mtu wa kulalamika
 • Asiwe mtumiaji wa kilevi chochote kile
 • Awe na tabia njema kwa ujumla

Ikiwa ungependa kuwa wakala wa vitabu na unakidhi vigezo hivyo hapo au una ndugu au rafiki mwenye vigezo hivyo hapo basi awasiliane nasi kwa njia zifuatazo:
Mikoa ya kipaumbeleni na idadi ya mawakala/wauzaji wanaohitajika Dar (10), Arusha (2), Mbeya (2)
Simu: 0763 071007 (call, sms &whatsapp)
Email: ushauri@kilimo.net

Mwisho wa kutuma maombi ni Jumatatu tarehe 21/08/2017
Pia tunakarisbisha wadau wenye bookshops na maduka ya pembejeo ambao wangependa kuwa washirika (partners) kwenye uuzaji wa vitabu hivi wanakaribishwa sana.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *