Zawadi ya KITABU cha Kilimo kwa Mwezi August 2017

Zawadi ya KITABU cha Kilimo kwa Mwezi August 2017

Habari mjasiriamali wa kilimo, Hongera kwa mapambano ya kusaka mafanikio kupitia Kilimo. Tunafurahi sana kufanya kazi pamoja na Wewe, hususani kwenye eneo la kupeana maarifa ya kilimo biashara. Lengo letu ni kuhakikisha unapata maarifa ya kutosha yatakayokuwezesha kufanya kilimo cha faida, na sio kilimo cha kubahatisha.
Kabla mwezi huu wa 8 haujaisha, tunapenda kukuletea kitabu kizuri sana, kinafundisha kuhusu Teknolojia za
Utayarishaji, Usindikaji na Hifadhi ya Mazao ya Nafaka baada ya Kuvuna
https://dl.dropboxusercontent.com/s/l0al8mlblluayvh/mazao%20ya%20nafaka-book%201.pdf?dl=0
Ukishabonyeza hiyo link hapo, hicho kitabu kitajidownload, hivyo unaweza kucheki kwenye folder la Downloads ambalo linatunza mafile ya kudownload.

MUHIMU: Ili kupata vitabu vingine vizuri, machapisho ya kilimo, audio na video za mafunzo ya kilimo, ufugajina masoko, tumetengeneza Maktaba ya Kilimo ya mtandaoni (Kilimo Online Library)
Maktaba hiini sehemu pa kuweka na kuhifadhimasomo ya kilimo biashara ambapo mtumiaji anaweza kuingia wakati wowote na kukuta masomo (materials) yake yapo palepale, pia hata simu ikipotea anaweza kuingia kwa simu nyingine au computer na akaweza kujisomea masomo yake bila shida yoyote. Kwa vile ni ya mtandaoni (online) haichukui nafasi kwenye simu yako, hata kama material yana ukubwa gani unaweza kuaccess kupitia simu yako hata kama simu yako memory yake ni ndogo.
Kwa sasa tumeanza na masomo ya Kilimo, ila kwa baadaye tutaendelea na Nyanja nyingine.
Kila Mwezi kutakua na masomo mapya yatakua yanawekwa kwenye Maktaba (Library) hii. Makataba hii tayari imeshaanza kufanya kazi, kwa wale waliojiunga na program yetu ya Kilimo Uhakika tayari wanajifunza kwenye maktaba hii. Kwa sasa kuna masomo mengi ya kilimo, masoko na ufugaji tayari yameshawekwa. Pia tumeongeza vitabu vya OFA vinavyohusiana na mafunzo ya uongozi, biashara, fedha, hamasa nk. Tayari Audio books (Vitabu vya kusikiliza kwa njia ya sauti) zaidi ya 40 zimeshawekwa kwenye maktaba hii. Hapa chini tumekuwekea picha chache za kuonyesha makataba yetu ikiwa katika hatua za awali.

Huo ni mwenekano wa sasa wa Masomo yaliyopo mpaka sasa. Tuendelea kuongeza masomo


Hapo Juu ni Muonekano wa baadhi ya masomo kuhusu Vitunguu maji


Kwa wale wapenzi wa kujisomea vitabu na kusikiliza audio books za mafunzo kuhusu ujasiriamali, fedha, uongozi n.k wataweza kupata vitabu na audio za kutosha kabisa


Ili kuweza kujiunga na library hii utabidi kuwa na vitu vifuatavyo:
1. Unapaswa uwe na email. Kutokana na mfumo tunaotumia kwa kuanzia inabidi uwe na email ya gmail.
2. Uwe na smart phone au computer ambayo utaweza kuitumia kuingia
3. Ada ya mwaka ambayo ni 30,000 au Ada ya mieizi 6 ambayo ni 20,000.
Namna ya Kujiunga: Unalipia Ada ya 30,000 (ada ya mwaka) au 20,000 (ada ya miezi 6). Unachagua unataka kulipa ya muda gani. Malipo yanafanyika kwa MPESA namba 0763 071007 au TIGO PESA namba 0712578307 (Jina litaonyesha Daudi Mwakalinga). Ukishafanya malipo utatuma Meseji (SMS au WHATSAPP) yenye Jina na email yako kwenye namba 0763 071007
Kwa Maelezo Zaidi wasiliana nasi kwa:
Simu: 0763 071007
Email: ushauri@kilimo.net

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *