SEMINA YA KILIMO BIASHARA KWA NJIA YA MTANDAO

SEMINA YA KILIMO BIASHARA KWA NJIA YA MTANDAO

Habari ndugu mjasiriamali wa Kilimo, ni matumaini yetu kwamba unaendelea vyema na mapambano ya kuelekea kwenye mafanikio. Mtandao wa Kilimo Biashara (kilimo.net) unatarajia kuendesha mafunzo ya kilimo na masoko kupitia mtandao wa barua pepe (email) na WhatsApp. Mafunzo yatakua ya siku 5 ambapo kila mshiriki ataweza kupata masomo kuhusu  Masoko na Kilimo kwa mazao matano Nyanya, Vitunguu maji, Tikiti maji, Mahindi na Mpunga.
Kwanini Semina kwa njia ya Mtandao:
Ni ukweli usiopinga kwamba ukuaji wa teknolojia umerahisisha mambo mengi sana, ikiwapo swala la kujifunza. Sasa hivi unaweza kutumia simu, au kompyuta kujifunza mambo mengi sana, vijana wengi na hata wasio vijana wanatumia simu zao na vifaa vingine kujifunza mambo mbalimbali kupitia intaneti, moja ya mambo hayo ni Kilimo. Kutokana na mwamko huo ndipo tulipoona haja ya kuanzisha mtandao wa kilimo.net ili kuwafikishia wakulima elimu ya kilimo biashara kupitia mtandao wa intaneti. Kwa sasa tunawafikia maelfu ya wakulima kila wiki wanaopata mafunzo na taarifa mbalimbali kuhusu masoko na kilimo. Hivyo tuliona njia nzuri ya kuwafikia wakulima wengi  kwa mfunzo ya kina ni kuandaa semina kupitia mtandao ambapo mshiriki wa semina atapatiwa mafunzo kupitia email yake pamoja na  kupitia mitandao mingine kama Telegram au Whatsapp.
Ufinyu wa muda. Sababu ya pili, tuligundua kwamba wasomaji wetu wengi ni wafanya kazi na watu wenye shughuli kadha wa kadhaa, ambapo wanakua na muda mchache sana, kiasi kwamba ni ngumu kumwandalia semina ya siku kadhaa ahudhurie kila siku. Kutokana na changamoto ya muda, tukaona njia nzuri ni kuja na mafunzo ya mtandao, ambapo masomo yatatumwa kupitia barua pepe (email) ya mshiriki. Badala ya kuhudhuria semina ya siku mbili au tatu, ambapo atatumia masaa kadhaa kusafiri na mengine kukaa darasani, tukaona  tunaweza kuandaa masomo hayo kwa njia ya maandishi, audio na video na kumfikishia mkulima popote pale alipo na akajifunza akiwa popote alipo.
Kwa njia ya email, mshiriki anaweza kuja kufanya rejea hata siku za mbeleni, pia badala ya yeye kwenda kuhangaika kutafuta masomo kwenye Google, badala yake masomo yanamjia moja kwa moja kwenye email yake na anaweza kuyahifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadae.
Gharama nafuu za kupata semina. Kwa sababu gharama kadhaa zitapungua na nyingine hazitakuwepo kabisa kama gharama za ukumbi, chakula n.k hivyo mshiriki anaweza kupata mafunzo haya kwa gharama kidogo.
Hizo ni baadhi ya sababu za kwanini tumetumia njia ya mtandao kuwafikia wakulima kwa Semina ya Kilimo Biashara.
Baadhi ya Masomo na mambo mbalimbali Yatakayofundishwa na kujadiliwa kwenye Semina.

 • Mienendo ya masoko ya mazao kwa mwaka mzima. Hapa tutaweza kufahamu bei za mazao zinavyopanda na kushuka katika mwaka mzima. Mshiriki wa semina atafunzwa Miezi sahihi ya kupanda na kuvuna ili kupata bei nzuri. Pia kila mshiriki atapata Kalenda ya masoko ya mazao kwa hapa Tanzania.Kalenda yenye mazao zaidi ya 20
 • Mazao ambayo yana soko zuri kwa mwaka mzima.
 • Vigezo vya kuzingatia kwenye kufanya maamuzi ya zao gani  la kulima na mahali pa kulima hilo zao. Kwa wale ambao hawajui wafanye kilimo cha zao gani, watapata ufumbuzi hapa
 • Masoko makubwa ya Mahindi na Mchele kwa hapa Tanzania na kiwango masoko hayo yananachukua. Tutaangazia Makampuni makubwa yanayonunua zaidi ya asilimia 70 ya mahindi yanayouzwa hapa nchini. Pia utapata Mawasiliano ya baadhi ya masoko hayo
 • Mafunzo ya Kilimo bora cha Vitunguu Maji, Nyanya, Tikiti Maji, Mpunga na Mahindi. Hapa tutajifunza kuanzia kuandaa shamba hadi kuvuna, kuhifadhi na kupeleka sokoni.
 • Namna ya kupata taarifa za bei ya mazao kwenye masoko makubwa hapa nchini.
 • Mbegu bora 5 hadi 10 za mazao  kama mahindi, Nyanya, Vitunguu, Hoho, Mpunga, Tikiti maji. Aina ya mbegu ambazo ndio zinazopendwa sokoni.
 • Makampuni makubwa ya mbegu bora na namna ya kuweza kuyafikia, ili kupata mbegu halisi (original). Hii itakusaidia kuepuka mbegu feki, maana mbegu feki  imekua ni kilio cha wakulima wengi sana.

Kwa wale watakaokua wanahitaji mashamba ya kukodisha wataunganishwa na watu wenye mashamba.
Tarehe ya Semina: 29 May hadi 2 June  2017. (Jumatatu hadi Ijumaa)
Muda wa Kujiandikisha: Kuanzia tarehe 16 hadi 27 May 2017
OFA/ Bonus  zitakazotolewa wakati na baada ya mafunzo:

 • Vitabu 2 vya Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji Kitaalamu
 • Kitabu kizuri cha Usindikaji wa Mboga na Matunda (Maembe, Machungwa, Mananasi, Mapapai, Mapesheni, Maparachichi,  Ndizi, Kabichi, Kabichi za Kichina, Karoti, Mchicha, Nyanya, Vitunguu, n.k)
 • Kitabu kizuri cha Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Hifadhi ya Mazao ya Nafaka baada ya Kuvuna
 • Mwongozo wa Viwango Bora vya Mahindi: Uhakika wa Upatikanaji wa Soko zuri
 • Kalenda ya soko ya mazao 21. Hapa utafahamu miezi yenye Soko zuri kwa  hayo mazao yote 21.
 • Mwongozo wa Kulima Kitaalamu zao la Vitunguu Maji pamoja na Mchanganuo wa gharama na Faida (Cost Benefit Analysis – CBA) kwa zao la Vitunguu maji
 • Mwongozo wa Kulima Kitaalamu zao la Nyanya pamoja na Mchanganuo wa gharama na Faida (CBA) kwa zao la Nyanya
 • Mwongozo wa Kulima Kitaalamu zao la Tikiti maji pamoja na Mchanganuo wa gharama na Faida (CBA) kwa zao la Tikiti maji
 • Mwongozo wa Kulima Kitaalamu zao la Pilipili Hoho pamoja na Mchanganuo wa gharama na Faida (CBA) kwa zao la Pilipili Hoho (Master plan na CBA)
 • Mwongozo wa Kulima Kitaalamu zao la Vitunguu Swaumu pamoja na Mchanganuo wa gharama na Faida (CBA) kwa zao la Swaumu
 • Mwongozo wa Kulima Kitaalamu zao la Papai pamoja na Mchanganuo wa gharama na Faida (CBA) kwa zao la Papai

Gharama za Semina na Namna ya Kujiandikisha kwenye Mafunzo haya:

 • Gharama au Kiwezesho cha Semina hii ni Elfu Kumi (10,000/= tu). Mafunzo ya Semina pamoja na OFA hizo zote hapo juu zitapatikana kwa gharama ileile ya semina ( yaani 10,000/= tu).  Gharama hii ni ndogo sana ukilinganisha na mambo utakayoyapata kwenye Semina.
 • Malipo yanafanyika kwa mpesa kupitia namba yetu ya 0763 071007.
 • Ukishafanya malipo unatuma ujumbe (SMS) wenye Jina lako na Email yako kwenye namba hizo ulizofanyia malipo (0763 071007) au kupitia whatsApp. Hakikisha email unayotuma ni sahihi. Baada ya muda mfupi utapokea Ujumbe kwenye email yako, Ujumbe wa kukukaribisha kwenye SEMINA.

Walengwa wa semina:

 • Wafanya kazi wa aina zote wenye nia  ya kuwekeza kwenye Kilimo
 • Wajasiriamali wa aina zote wenye matarajio ya kuwekeza kwenye kilimo
 • Wakulima wadogo, wa kati na wakubwa wenye kuhitaji kuongeza maarifa ya kuhusu uwekezaji kwenye kilimo na masoko

Njia na mbinu za mafunzo zitakazotumika:

 • Makala za maandishi
 • Njia ya sauti (Audio)
 • Njia ya video (Vdeo za mafundisho)

Kwa kupata mafunzo haya ya semina na kuyafanyia kazi, FAIDA kwenye kilimo chako ni jambo la UHAKIKA
Karibu sana Kwenye Semina ya Kilimo Biashara.
0763 071007
ushauri@kilimo.net
www.kilimo.net
 

Response to "SEMINA YA KILIMO BIASHARA KWA NJIA YA MTANDAO"

 • Asanteni sana, nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuwafuatilia kwani mnanifumbua mambo mengi sana kuhusu kilimo ambayo mwanzo sikuyajua

 • Safi sana Binafsi napenda sana Kujifunza mabo ya Kilimo,huwa mnafanya semina za wazi!? ambazo sio za On Line!! kama zipo wapi!! na utaratibu ukoje!!??

 • Leave a Reply

  Your email address will not be published. Required fields are marked *