WAFAHAMU WALIMU WA SEMINA YA KILIMO BIASHARA KWA NJIA YA MTANDAO

WAFAHAMU WALIMU WA SEMINA YA KILIMO BIASHARA KWA NJIA YA MTANDAO

Habari ndugu mjasiriamali wa kilimo. Tukiwa tunaendelea na maandalizi ya semina ya kilimo biashara kupitia mtandao, tunapenda kuwatambulisha kwenu baadhi ya walimu watakao fundisha semina hii. Kusema kweli tumekuandalia walimu wazuri wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha kuhusiana na mada za semina. Kwenye semina hii kutakua na walimu wa 5, ila kwa leo tunaweka wasifu wa walimu wa 2 kisha kesho tutamalizia na waliobaki.

  1. ZABRON M. MSENGI

Zabron Msengi ni mtalaam wa kilimo ana shahada ya kilimo ya  Uzamili  ya Uzalishaji wa Mbegu bora za Mazao ( MSc in Plant   Breeding) kutoka Chuo kikuu cha Kilimo  Sokoine (SUA). Pia ana shahada ya kwanza ya Kilimo kutoka hapohapo chuo cha SUA. Kwa sasa anafanya kazi katika Kituo cha Utafiti cha Kilmo Selian.kilichopo Arusha kwenye Idara ya mahindi. Ni mtafiti mkuu msaididi wa Mazao. Ambapo kazi yake kubwa ni  uzalishaji wa mbegu bora za mahindi (Maize Breeder)  Ambazo zinaweza kutoa mavuno mengi, zenye ukinzani wa magonjwa ya mahindi kama vile mnyauko wa mahinndi (maize lethal necrosis) , milia ( maize streak virus)nk,  pia kutengeneza mbegu za mahindi zinazovumilia ukame. Hii inalenga kusaidia wakulima wetu kupata mbegu bora  ili waweze kujitosheleza kwa chakula na mahitaji mengine kama kusomesha nk..ukizingatia zao la mahindi linalimwa nchi nzima na siku hizi linatumika kuwakwamua wakulima wetu kama zao la chakula na biashara.
Kutokana na utaalamu na uzoefu wake katika zao la Mahindi, Mwalimu Zabron Msengi atakua akifundisha kwenye semina hii kuhusu kilimo cha mahindi kibiashara kuanzia uchaguzi wa mbegu, uaandaji wa shamba, utunzaji  hadi  mavuno. Pamoja na hayo pia washiriki watafundishwa kuhusu mbegu bora mpya zinazofanya vizuri kwenye kila kanda kutokana na hali ya hewa husika.

  1. RASHID MDOKA

Rashid Mdoka ni mtaalamu wa kilimo mwenye shahada ya kilimo toka chuo kikuu cha sokoine (SUA) Bsc. Agronomy yaani (sayansi ya kilimo yaani mazao na udongo). Kwa sasa ni mkugenzi wa kampuni ya  Kilimobero Agriculture Center ( KAC) ambayo inatoa huduma za pambejeo na ushauri wa kilimo kwa mkoa wa morogoro. Pamoja na kua mkurugenzi wa KAC, pia ana uzoefu wa kutosha katika kilimo cha mpunga na mahindi. Uzoefu wake aliupata katika kazi ya kufundisha wakulima WA kilimo cha mahindi na mpunga Kwa miaka Mitatu (2012-2015) kupitia mradi wa kimarekani unaoitwa USAID -NAFAKA feed the future Tanzania.  Mradi huu ulifanya kazi maeneo ya kilombero,  ulanga,  mvomero, kongwa na kiteto.  Pia amewahi kufanya kazi katika kampuni ya viwatilifu shambani ya Arysta Life science kwa miaka miwili (2015-2017). Mr. Rashid Mdoka ni moja kati ya walimu watakaofundisha kwenye semina hii, Yeye atajikita zaidi kwenye kilimo cha Mpunga kitaalamu na kibiashara.
Waalimu wengine watakaokuwepo  wasifu wao utafahamika kesho. Karibu sana.
Kama bado hujajiandisha na Semina, jitahidi kufanya hivyo, muda wa kujiandikisha unaelekea ukingoni. Mwisho ni tarehe 27 May 2017 (Jumamosi hii). Kiingilio cha Semina ni 10,000 pekee ambayo inalipwa kwenye namba 0763 071 007, kisha unatujulisha kwa sms yenye jina na email yako, kisha utaunganishwa moja kwa moja kwenye mfumo wetu.
Kufahamu zaidi kuhusu Semina bonyeza hii link hapa: http://kilimo.net/2017/05/17/semina-ya-kilimo-biashara-kwa-njia-ya-mtandao/
Karibu sana
0763 071 007
ushauri@kilimo.net

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *