WAFAHAMU WALIMU WA SEMINA -2

WAFAHAMU WALIMU WA SEMINA -2

Habari za leo mjasiriamali wa kilimo, leo tumekuletea awamu ya pili ya wasifu wa waalimu/wawezeshaji watakakaofundisha Semina ya Kilimo Biashara kupitia njia ya mtandao (online Training). Awamu ya kwanza tuliona wasifu wa walimu wawili, leo hii tunakwenda kuona  wasifu wa wawezeshaji 4. Fuatana nami hapa chni nimekuwekea orodha hiyo:

  1. MNADI TALIBO

Mnadi Talibo ni mtaalamu wa kilimo mwenye shahada ya uzamili katika  Kilimo ugani kutoka chuo kikuu cha Wageningen nchini Uholanzi (Msc. Agricultural extension ) , ana shahada ya sayansi kilimo kutoka Chuo kikuu cha kilimo Sokoine (Bsc. Agricultural General ) amepata mafunzo ya muda mfupi kutoka nchini Misri katika masuala ya maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia teknolojia mpya za kilimo cha umwagiliaji , pia amepata mafunzo ya muda mfupi nchini Japan katika masuala ya kilimo bora cha zao la mpunga . Ni Afisa kilimo Mwandamizi katika (Senior Agricultural Officer ) katika Wizara ya maji na umwagiliaji kituo chake cha Kazi ni  ofisi ya umwagiliaji kanda ya Mbeya ana uzoefu wa Kazi za kilimo kwa muda wa miaka 10 aliajiriwa mwaka  2007 mpaka sasa kwa Kazi hiyo masuala ya kilimo,  ni mtaalam katika mazao ya mbogamboga na matunda (horticultural crops) k.m vile vitunguu, matikiti, nyanya, pilipili hoho nk pia ni mtaalam wa mazao ya nafaka k.m mpunga , mahindi ,mtama nk na pia zao kama alizeti. Anatoa ujumbe kwa washiriki kwamba kilimo kinachofuata ni kilimo shadidi cha mpunga (System of Rice Intensification) ni teknolojia ya kulima mpunga kwa kutumia maji kidogo ( unapunguza matumizi ya maji kwa 50% ) na kupata mavuno mengi 8 tani kwa hekta sawa na gunia 40 kwa ekari au zaidi. Mwezeshaji Mnadi Talibo atafundisha teknolojia ya kilimo shadidi cha mpunga.

  1. DANIEL KABAKA.

Daniel Kakaba ni mtaalam wa kilimo kutoka chuo kikuu cha sokoine (SUA) ana shahada ya kilimo cha bustani, (Bsc. Horticulture) na amebobea katika maswala yote ya kilimo cha bustani (mbogamboga) aina zote, matundanakilimo cha mazao ya viungo. Daniel ana uzoefu wa zaidi ya miaka 3 kwenye sekta ya kilimo na kwa sasa anafanya kazi na Kampuni ya Mbegu ya East West (East West Seed Company) kama Afisa Utafiti wa kanda ya ziwa. Moja ya kazi zake kubwa ni kufanya majaribio ya mbegu na kuwafunza wakulima na kuwashauri mbegu bora zinazofaa kutokana na majaribio ya mbegu anayoyafanya  Taasisi na kampuni nyingine ambazo amewahi kufanya kazi ni pamoja na TCCIA (Tanzania chamber of commerce industry and agriculture), BESA HERITAGE FARM n.k. Pia Mr Daniel ni mkulima wa mazao ya bustani kama Tikiti maji na Vitunguu. Mwalimu Daniel Kwenye semina hii atatoa mafunzo ya kina kuhusu kilimo cha Vitunguu na Tikiti maji

  1. ANANIA JOSIA

Anania Josia ni Mtaalamu wa kilimo, anayo shahada ya Kilimo cha bustani (BSc. Horticulture) kutoka Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Amewahi kufanya kazi na Mradi wa Kukuza thamani ya kilimo(USAID/TAPP) Kama Mtaalamu wa kilimo (Agronomist) kwa miaka mitatu. Kwa sasa anafanya kazi na Kampuni ya utafiti na utengenezaji wa mbegu chotara (Rijk Zwaan-Afrisem) Kama Mtaalamu wa Kilimo na Mauzo ya Mbegu (Product Development Specialist) kanda ya Kasikazini ya  Mashariki. Ambapo kazi Kubwa ni kuhakikisha anaondoa changamoto kubwa mbili ya upatikanaji wa mbegu bora na Kutoa Elimu ya kilimo cha kisasa (Ndani na Nje ya Greenhouse) kwa wakulima ili kuinua kipato cha Mkulima na Kutengeneza wakulima wataalamu. Ukiacha kua  Mtaalamu, lakini vilevile Ndugu Anania ni mkulima mzoefu wa kilimo cha mazao ya mboga kama vitunguu, Nyanya, Hoho n.k. Mr. Anania atafundisha kilimo cha nyanya, kuanzia upanzi hadi kuvuna.

  1. DAUDI MWAKALINGA

Daudi ni mtaalamu wa kilimo na masoko. Anayo shahada ya kilimo cha bustani (Bsc. Horticulture) kutoka chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA). Daudi ana uzoefu wa zaidi ya miaka 5 kwenye sekta ya kilimo, amewahi kufanya kazi na kampuni ya Kimataifa ya Enza Zaden inayojihusisha na uzalishaji wa mbegu chotara za mbogamboga (Vegetable hybrid seeds) Pia amefanyakazi na taasisi ya Farm Concern International (FCI)  kama Meneja wa masoko na Biashara (Markets and Trade Manager), FCI inajihusisha na kuwatafutia masoko wakulima wadogo. Daudi Mwakalinga ndiye mwanzilishi wa mtandao wa kilimo biashara (kilimo.net) unaotoa mafunzo ya kilimo na masoko kwa wakulima. Amewahi kufanya mafunzo ya kilimo na masoko kupitia radio  (kama vile Radio NURU FM, Manyara FM, Sunrise Radio nk ) na magazeti kama Mtanzania, Upendo nk Ndiye mwandishi mkuu wa makala za ushauri wa kilimo kwenye mtandao wa kilimo.net. Pia ni mshauri (consultant) wa kilimo biashara ambapo hufanya mafunzo kwa taasisi na makampuni mbalimbali, wakulima wadogo, wakati na wakubwa. Kwenye Semina hii ndugu Daudi atajikiata zaidi kwenye mada zinazohusu masoko na biashara.

Muhimu sana: Kama Bado Hujajiandisha na Mafunzo haya leo ndio siku ya Mwisho ya Kujiandikisha, wahi kabla muda haujaisha. Kiingilio cha Semina ni 10,000 pekee ambayo inalipwa kwenye namba 0763 071 007, kisha unatujulisha kwa sms yenye jina na email yako, kisha utaunganishwa moja kwa moja kwenye mfumo wetu.

Kufahamu zaidi kuhusu Semina bonyeza hii link hapa: http://kilimo.net/2017/05/17/semina-ya-kilimo-biashara-kwa-njia-ya-mtandao/

Response to "WAFAHAMU WALIMU WA SEMINA -2"

  • Hongereni kwa maono haya mazuri. Chuo cha Mugerezi Spatial Technology – MUST College kilichopo Dar es salaam kwa sasa kinashirikiana na VETA kutayarisha mtaala wa Kilimo Biashara ngazi ya VETA ambao pia utaingiza ujuzi wa Teknolojia za Geographic Information System (GIS) na GPS na Mobile Mapping. Kozi itajulikana kwa jina la Geo Agrobusiness. Ujuzi wa GIS utakaoingizwa kwenye mtaala utawawezesha wahitimu pamoja na mambo ya kilimo na biashara, wataweza:
    (a) Kupima mashamba yao na kujua mipaka na eneo
    (b) Kupima na kujua umbali toka sehemu moja hadi nyingine
    (c) Kutengeneza ramani za miinuko (DEM-contouring) kutoka kwenye picha za satellite
    (d) Kujua walipo wateja na watoa huduma kama vile pembejeo (customer mapping)
    (e) Kutumia simu za mkonomi kukusanya na kusambaza taarifa mbali mbali za kilimo na mazao
    (f) Kutumia teknolojia ya Computer na Internet kibiashara.
    Tunahitaji kupata mawazo na ushauri ya wataalamu wa KilimoBiasharaambao nimewasoma humu ndani. Naomba mawasiliano jinsi ya kuonana ana kwa ana. Simu yangu 0764 885989; email edwin.mugerezi@infobridge.co.tz

  • asante sana kwa elimu nzuri juu ya kilimo binafsi nimepata kitu kipya kitanisaidia ktk kilimo changu

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *