Semina ya Kilimo: Wahi Nafasi Hii ya Upendeleo
Habari ndugu Mjasiriamali wa Kilimo,
Semina yetu ya Kilimo Biashara kupitia njia ya Mtandao, tayari imeshaanza tokea jumatatu, na washiriki wana hamasa kwelikweli, Watu waliojitokeza ni wengi, tunawashiriki zaidi ya 300. Masomo yameanza vizuri na yanaendelea kikubwa na washiriki wanapata mafunzo haswa. Siku ya Kwanza tu tulipata simu za vituo viwili vya redio vikitamani kufanya interview na waandaaji kwa sababu ya mafanikio yaliyoonekana ya kuweza kupata washiriki zaidi ya 300 kwa semina ya kwanza. Tunamshukuru Mungu kwa mwitikio huo mzuri na hamasa waliyonayo washiriki ya kujifunza. Hata hivyo wapo watu wengi ambao bado wamekua wakituandikia sms na email hata kupiga simu kuulizia kama wanaweza kulipia, hata angalau washiriki mafunzo kwa siku zilizobakia. Hii ni kutokana na wengine kuchelewa kupata tangazo na email zetu, wengine walikua mbali sehemu ambapo network hakuna, wengine mwisho wa mwezi ndio wanakua vizuri kifedha, na sababu kadhaaa ambazo kusema kweli tumeona zina mashiko. Kwa sababu hiyo tumeona tutoe nafasi ya Upendeleao kwa wale ambao wangependa kushiriki siku zilizobaki au pia wangependa kupatiwa mafunzo yaliyofundishwa na yanayoendelea kufundishwa. Tumeandaa vizuri masomo yote yaliyofundishwa (maandishi, Audio na Video), ili kwa Yule ambaye alishindwa kushiriki semina hii kwa namna yoyote basi ataweza kupata mafunzo yote yaliyotolewa.
Rafiki yangu, ikiwa wewe ni mmoja ya waliotamani kushiriki ila kwa sababu kadhaa ulishindwa kuwahi semina hii, basi tunakupa nafasi ya Upendeleo ya kupata mafunzo hayo. Ikiwa utaweza kujiunga leo na Kesho basi utapata fursa ya kuungwa kwenye kundi la whatsapp ambapo utashiriki pia mijadala ya maswali na majibu. Wahi sasa usichelewe tena.
Ili kupata masomo hayo unafanya malipo ya 10,000/= tu kwa namba yetu ya mpesa 0763 071007 (Jima litaonyesha Daudi Mwakalinga). Ukishafanya malipo unatuma ujumbe (SMS) wenye Jina lako na Email yako kwenye namba hizo ulizofanyia malipo (0763 071007) au kupitia whatsApp. Baada ya muda mfupi utapokea Ujumbe kwenye email yako, Ujumbe wenye masomo ya SEMINA. Nafasi hii ya Upendeleo itakua wazi kwa wiki moja tu kuanzia leo (31 May 2017) mpaka 7 June 2017. Baada ya Muda huu kuisha masomo haya yatapatikana kwa gharama ya 40,000/= Karibu sana
Kama Ungependa kuelewa kwa kina Kuhusu Semina hii Ya Kilimo Biashara kupitia njia ya Mtandao, basi Bonyeza hii Link hapa: http://kilimo.net/2017/05/17/semina-ya-kilimo-biashara-kwa-njia-ya-mtandao/
Daudi Mwakalinga
0763 071007
Response to "Semina ya Kilimo: Wahi Nafasi Hii ya Upendeleo"
Habari, nililipia gharama za kushiriki semina lakini sijapata kinachojiri kwenye semina tangu mmeanza,