Jipatie Miche Bora ya Matunda MbaliMbali
Jipatie Miche Bora ya Papai, Michungwa, Miembe, Miparachihchi, Pesheni (passion), Limao, Mipera n.k.
Tunayo Miche ya Papai ya aina mbalimbali: Mipapai mifupi yenye rangi nyekundu ndani, mipapai mifupi yenye rangi ya njano ndani na mipapai ya kienyeji: Mipapai hiyo mifupi (nyekundu na njao) inaanza kuzaa kuanzia miezi mitatu toka kupandikiza.
Miembe ntuliyonayo ni ile mifupi iliyofanyiwa Grafting. Miaka 3 tu inaanza kutoa matunda. Tofauti na ile mingine inayochukua miaka 7 kuanza kutoa matunda. Aina zilizopo ni Kenti, Red Indian, Apple, Bolibo, Dodo n.k
Michungwa na Miparachichi ipo pia ile ya muda mfupi (miaka 3 unaanza kuvuna).
Kipindi hichi cha mvua ndio kizuri kwa kupanda, kwasabau miche itastawi vizuri maana maji yapo, na pia itapunguza gharama za umwagiliaji.
Kitalu chetu cha miche kipo Morogoro mjini: Ila kwa anayechukua miche kuanzia 100 popote alipo Tanzania anatumiwa.
Bei za Miche:
Miche ya Papai: Papai fupi (nyekundu ndani), mche ni 4,000, Papai fupi (ndani njano) mche ni 3,000/=, Papai ya Kienyeji mche ni 2,000/=
Miche ya Michungwa, Miembe na Miparachichi: Mche mmoja 3,000/=
Miche ya Pesheni (passion), Limao, Mipera na mitopetope: mche ni 2,000/=
Karibu sana.
Mawasiliano: 0763071007
Email: ushauri@kilimo.net
Response to "Jipatie Miche Bora ya Matunda MbaliMbali"
Salaam,nipo dar,nataka miche mchanganyiko ya 50elf,naweza tumiwa dar?0714440554/0782004004. Ludovick.
Mnapatikana wapi? au inaweza kutumwa mikoa mbalimbali mfano Mimi nipo Dodoma
Habari ndg, me naona pia mngejaribu kuwasaidia wateja wenu wa miche kwa kuwaongoza ni wapi wanaweza kuuza bidhaa zao kwa bei yenye tija na kuwapa bei elekezi nadhani ingewasaidia hata nyiye wenyewe kuongeza soko la usambazaji wa miche.
Ni kazi nzuri nimeipenda sana nipo dar cijui ntapataje hizi mbegu nzuri za papai na embe na kama apple zipo nitafurahi pia na chungwa pamoja na mananasi
habari,
samahani kama ntakuwa nje ya maada ila mi nahitaji kupata elimu na miche ya limau,mwongozo tafadhari
Ndugu nimefurahi Sana kuiona website hii na uzuri nilishanunua nunua miembe,michungwa,mpomelo michache niiloipanda nyumbani japo nakosa utaalamu wa kukabili magonjwa.