Jipatie Mwongozo wa Kilimo Bora cha Papai

Jipatie Mwongozo wa Kilimo Bora cha Papai

Habari ndugu,,

Leo nakuletea somo kuhusu kilimo cha papai. Kilimo cha Papai ni fursa ambayo imeanza kukua kwa kasi siku za hivi karibuni na watu wameanza kuingia kwenye fursa hii. Kazi yangu ni kukuletea fursa hizi na kukupa ushauri wa kitaalamu. Mwishoni mwa somo nimekuwekea stori ya mkulima anayetengeneza milioni 10 kwa wiki, kwa kilimo cha Papai.

Utangulizi:
Mapapai ni zao moja kati ya mazao ya matunda yenye vitamini A na madini ya kalsiamu kwa wingi. Inaamanika asili ya papai, ni huko nchi za Amerka ya kati, (Mexico), ndipo zao ili likasambaa duniani kote. Kwa sasa zao hili hulimwa karibu kila mahali hapa nchini. Papai ni moja ya mazao yenye faida kubwa na yenye soko la uhakika. Ekari moja ya papai ikitunzwa vizuri inaweza kukupatia faida ya zaidi ya milioni 20 kwa kipindi cha miaka 2 hadi 3.

Aina za Papai
Zipo aina 3 za papai. 1. Papai dume (hizi hua zinatoa maua ya kiume na hua hazitoi matunda) 2. Papai yenye maua ya kike tu  hutoa matunda ya mviringo 3. Papai yenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite), matunda yake hua marefu.


Kuna aina 3 za mbegu za papai.

1. Mbegu za kienyeji (local varieties). hizi ni aina ya papai za kienyeji ambazo, mara nyingi hazifahamiki majina yake. Mbegu zake huwezi zipata kwenye mfumo rasmi wa mbegu (madukani) nk. mara nyingi mbegu hizi hupatikana kwa kuchukua matunda yaliyoiva na kuchukua mbegu zake.. kiswahili cha mtaani husema mbegu za kukamua. Miche ya mbegu hzi hupatikana kwa bei rahisi (1,000 hadi 2,000 kwa mche). Ukiwa unataka kulima kibiashara usitumie mbegu/miche ya namna hii, mara nyingi mavuno yake hayatabiriki, na mipapai dume huwa mingi ( Asilimia 30 hadi 50 huweza kuwa midume). Mipapai dume haitoi matunda.

2. Aina za kawaida au kwa kitaalamu hutulikana kama OPV yaani Open Pollinated Varieties. Hizi ni zile ambazo zimechavushwa kwa njia ya asili. Mbegu zilizochavushwa kiasili huzalishwa katika mazingira ambayo uchavushaji hausimamiwi, na matokeo yake ni mbegu huwa na tabia zinazotofautiana. Pia uzao wake ni wa wastani.  Mfano wake ni kama Calina. Bei ya mche hua kati ya 2,000 hadi 3,000 kwa mche.

3. Chotara (hybrid). Mbegu chotara huzalishwa katika mazingira yanayosimamiwa kwa uangalifu sana. Ushavushwaji hufanywa kati ya wazazi tofauti kwa lengo maalumu ya kupata tabia bora, ambazo zinatakwa na mkulima. Kwa vile uzalishaji unasimamiwa kwa uangalifu, kiwango cha ubora kiko juu kuliko mbegu zinazochavushwa kiasili. Mfano Malkia F1, Sinta F1, Red royal nk. Hizi hufanya vizuri maeneo mengi.. hua na uzao mkubwa kuliko aina nyingine tulizojifunza hapo juu. Gharama ya mche mmoja huwa kati ya 3,000 hadi 5,000

MAMBO YA KUZINGATIA WAK ATI WA UZALISHAJI:
Ili kupata mazao yenye ubora unaotakiwa ni muhimu kuzingatia kanuni za kilimo bora za uzalishaji
wa mapapai. Ubora wa matunda baada ya kuvunwa hutegemea jinsi yalivyozalishwa.

Baadhi ya kanuni hizo ni kama zifuatazo:
Kuchagua aina bora. Chagua aina bora ya kupanda kulingana na mahitaji ya soko.
Kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu Mapapi hushambuliwa kwa urahisi na magonjwa na wadudu, hivyo ni muhimu kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kugundua dalili za mashambulizi.
Endapo kuna dalili za mashambulizi, dhibiti mapema ili kuzalisha mazao bora yanayoweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.

Pia hakikisha shamba na barabara zake ni safi wakati wote ili kurahisisha uvunaji na
usafirishaji.

Maandalizi kabla ya kuvuna
Kukagua shamba. Kagua shamba kuona kama kuna mapapai yaliyokomaa
Mapapai hukomaa katika kipindi cha miezi minne hadi mitano kutoka maua yanapochanua.

Dalili za mapapai yaliyokomaa
Tunda hubadilika rangi kutoka kijani kibichi na kuwa ya kijani nyepesi hadi manjano.
Kuandaa vifaa vya kuvunia, kufungashia na kusafirishia

Vifaa vya kuvunia ni:
Vichumio
Mifuko
Ngazi

Vifaa vya kufungashia ni:
Makasha ya mbao/ plasitiki au makaratasi magumu

Vyombo vya kusafirishia ni:

  • Mikokoteni
  • Magari
  • Matela ya matrekta

Kuvuna.

  • Uvunaji bora wa mapapai ni wa kutumia mikono ambapo tunda huchumwa kwa mkono au kwa kutumia vichumio maalumu.
  • Vuna mapapai yaliyokomaa tu
  • Vuna mapapai pamoja na vikonyo vyake
  • Vuna kwa uangalifu ili kuepuka kudondosha matunda
  • Matunda yakidondoka, huchubuka, hupasuka au hupondeka hivyo husababisha upotevu.
  • Weka mapapai kivulini mara baada ya kuvuna

Kuchambua, Kusafisha na Kupanga Madaraja:
Ni muhimu kuchambua mapapai ili kutenga yaliyooza, kupasuka na yenye dalili za magonjwa au kubonyea. Lengo la kuchambua ni kupata matunda yenye ubora kulingana na matumizi , kwa mfano kusindika, kuuza au kusafirisha. Matunda yaliyooza na yenye wadudu ni vyema yafukiwe ili kuangamiza wadudu waharibifu na vimelea vya magonjwa, na pia kuzuia kuenea kwa wadudu na magonjwa hayo. Matunda yaliyopasuka, kubonyea au kuchubuka kidogo yatumike haraka kwa kuliwa. Matunda mazuri ambayo hayajapata madhara yoyote yatumike kwa ajili ya kusindika, kuliwa, kuuzwa au kusafirishwa.

Mwongozo wa Kulima Papai (Master Plan)
Tumekuandalia Mwongozo (Master plan) wa Kilimo hichi, utakaokuongoza hatua kwa kwa hatua kuanzia namna ya kuandaa shamba, kuchimba mashimo, upandaji kwa kutumia miche bora, kudhibiti magonjwa na wadudu kwa kupiga dawa, kuweka mbolea, kumwagilia na mengi mengi.
Hapa chini nimekupa kionjo tu cha baadhi ya mambo utakayoyakuta kwenye Master Plan ya kilimo cha Papai.

Baadhi ya Yaliyomo kwenye Mwongozo (Master Plan):
Uandaaji wa mashimo kitaalamu, na namna ya kutengeneza mchanganyiko mzuri wa udongo, mbolea, majani makavu na majivu.
Programu ya upigaji dawa za magonjwa na wadudukuanzia mwanzo hadi mwisho. Hapa tumependekeza dawa zenye ufanisi mzuri kwenye kudhibiti magonjwa na wadudu wasumbu kwenye mipapai.  Wale wadudu weupe wasumbufu, ambao huweka utandao mweupe (Kitaalamu huitwa White mealybugs), tumeweka dawa nzuri yenye kuwamaliza kabisa. Hivyohivyo kwa magonjwa na waududu wengine Muongozo huu unapendekeza dawa  zake na namna ya kuzipiga
Programu ya Uwekaji Mbolea:kuanzia mbolea ya kupandia hadi mbolea za kuimarisha matunda kua na ngozi imara. Wakati gani wa kuweka mbolea hizo, na  kiwango cha kuweka kwa mmea. Pia utajua namna ya kuchanganya mbolea mbili kwa uwiano mzuri wenye kuleta matokeo mazuri.
Programu ya Mbolea za majani (Booster):hapa utazifahamu mbolea zote za majani kuanzia za wakati mimea ni midogo hadi zile za kipindi cha matunda. Ili kuleta ufanisi zaidi tumeonyesha namna ya kuchanganya mbolea hizi za majani (boosters) na dawa za wadudu
Programu ya Umwagiliaji:Hapa utafahamu kiwango cha maji kinachohitajika kwenye kila hatua ya ukuaji ya mipapai. Pia utafahmu ni wakati gani wa kumwagilia kila siku, kila wiki na ratiba ya mwezi.
Shughuli nyingine zote muhimu zipo, na zimewkwa kwa mtiririko mzuri ambao kila mkulima ataelewa na kuweza kutekeleza ipasavyo.

Gharama ya Muongozo (Master Plan)
Kwa sasa Mwongozo huo unapatikana kwa bei ya OFA ya 20,000 tu. Pia OFA hiyo itaambatana na kupatiwa Mchanganuo wa Gharama na FAIDA (Cost Benefit Analysis au CBA) kwa zao la Papai. Ofa hii mwisho ni 30 June 2018. Baada ya muda wa ofa kuisha Mwongozo huu utapatikana kwa gharama ya 50,000.

Namna ya Kupata nakala yako ya Mwongozo:
Unafanya malipo ya 20,000 Kwa mpesa 0763 071007 au Tigo pesa 0712578307 (Jina Litaonyesha Daudi Mwakalinga)
Ukishafanya malipo unatuma Ujumbe wenye Jina na email yako kwenda 0763 071007 au 0712 578307. Kama huna email na ungependa kutumiwa Kitabu kwa Whatsapp au Telegram basi utatuma ujumbe WhatsApp au Telgram kwenda namba 0763 071007
Karibu sana
Daudi Mwakalinga
0763 071007
Email: ushauri@kilimo.net

 

Mkulima anayetengeneza milioni 10 kwa wiki:

Wiki chache zilizopita nilipigiwa simu na mkulima mmoja ambaye yupo Mkuranga. Mkulima huyu amelima ekari 7 za papai aina ya Malkia F1. Tayari ameanza kuvuna kama mwezi mmoja uliopita. Kwenye ekari 7 anavuna tani 20 kila wiki (yaani kilo 20,000). Soko lake ni wenye viwanda vya usindikaji na wachuuzi wengine ambao hufika hadi shambani. Kwa sasa bei ni TZS 500 kwa kilo. Hivyo kwa wiki anatengeneza 500 x 20,000 (tani 20) = 10,000,000 (milioni 10) Hii ni kwa wiki pekee, Kwa Mwezi je? Kwa Mwaka je? Unaweza kuona namna kilimo hichi kinalipa.

 

Miche ya Papai fupi za kisasa.  Aina tulizo nazo kwa sasa ni Malkia F1 na Calina.  Wahi ujipatie kwa bei ya OFA ya 3,000 tu kwa mche badala ya 5,000. Hii ni miche original, na sio ya kukamua.

Ukiwa unahitaji kutembelewa shambani kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu, kupima udongo, nk. wasiliana nami kupitia 0763 071007.

Ikiwa unayo mtaji wa kuwekeza kwenye kilimo ila unataka ushauri uwekeze kwenye kilimo cha zao gani pia usisite kunicheki.

Asante sana

Daudi Mwakalinga

0763 071007

www.kilimo.net

Response to "Jipatie Mwongozo wa Kilimo Bora cha Papai"

  • Kumekuwa na wimbi kubwa sana la matapeli, ambao huandaa nakala mbalimbali za mafunzo na hutumia njia kama hii yakutaka pesa itumwe ili mlengwa (anayehitaji huduma) aweze kupatiwa. Na mwisho wa siku watu wanaishiwa kutapeliwa. Je, unatuhakishia vipi usalama wa pesa zetu baada ya kutuma na kutaka masomo au huduma hii uliyosema?

  • ahsante ndg Daudi Mwakalinga kwa maelezo yako mazuri.na yenye kutia matumaini. Naomba kuuliza jee endapo mimi mkulima mdogo mdogo na ambae ni vusiwani Zanzibar vipi nitaweza kupata mbegu za hio Malkia F1 badala ya miche na ni kiasi gani kwa pakti moja ya mbegu na kwa wastani ndani ya pmakt moja muna mbegu ngapi?

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *