Habari ndugu mkulima mwenzangu, ni matumaini yangu unaendelea vyema katika safari ya kusaka mafanikio. Kitu cha muhimu sana unachopaswa kufahamu ni kwamba Mafanikiokatika jambo lolote hutegemea sana na kiwango cha MAARIFA kwenye jambo husika. Hata mafanikio kwenye kilimo yanategemea sana na maarifa uliyonayo kuhusu kilimo husika. Hivyo basi usiache kujifunza mara kwa mara. Ni heshima kwangu kupata fursa hii ya kua mwalimu na kocha wako wa masuala ya kilimo biashara kupitia blog hii ya Kilimobiashara (www.kilimo.net). Leo tunakwenda kujifunza kuhusu MBINU ZA MSINGI ZA KUTHIBITI MAGONJWA NA WADUDU KATIKA KILIMO CHA MBOGA. Japo mafunzo yameongelea zaidi kudhibiti magonjwa na wadudu kwenye mboga, lakini mbinu nyingi hapa zinatumika pia kwenye mazao mengine, nafaka, mikunde, matunda n.k Karibu sana.
Madhara ya magonjwa na wadudu
a) Hupunguza kiasi cha mavuno na hata kuua mimea kabisa.
b) Hupunguza ubora wa mboga.
c) Huongeza gharama za uzalishaji, hasa madawa ya viwandani yanapotumiwa.
d) Huongeza uharibifu wa mboga baada ya kuvuna.
Namna ya kutambua magonjwa na wadudu washambuliao mboga:
Lazima utambue aina ya ugonjwa au mdudu ili utumie kinga ianayostahili. Hii siyo kazi rahisi. Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo unaweza kutumia:
a) Kutumia uzoefu wako, hasa baada ya kuwa na wataalam wa wadudu na magonjwa ya mimiea kwa muda mrefu.
b) Kutumia mabwana shamba.
c) Kutumia wataalam wa magonjwa na wadudu wa mboga.
d) kuchunguza sehemu ya mmea uliyougua kwenye maabara.
Kanuni za kukinga mboga dhidi ya magonjwa na wadudu
Kabla hujaamua kutumia madawa ya kienyeji au viwandani, hakikisha unafanya mambo yafuatayo hatika bustani yako:
Chagua udongo usiokuwa na magonjwa ya mboga unayotaka kuzalisha.
Tumia mbegu bora, kwani baadhi ya magonjwa hutokana na mbegu.
Hakikisha kuwa vitalu, bustani na sehemu ya kuhifadhi mboga ni safi. Uchafu na magugu huvutia magonjwa na wadudu waharibifu.
Toa majani au mimea iliyokwisha ugua, na ichome moto au ifukie.
Panda mazao muda unaotakiwa ili kukwepa baadhi ya magonjwa ya msimu.
Epuka kupanda mboga ya jamii moja katika eneo moja kwa misimu mingi mfululizo. Mfano Nyanya, Pilipili Hoho, Ngogwe na Viazi mviringo ni jamii moja ya Solanaceae. Mazao haya hayapaswi kupandwa eneo moja kwa misimu mfululizo.
Changanya mazao au mimea ambayo inafukuza magonjwa na wadudu kama vile mimea inukayo.
Epuka kuchanganya mboga na baadhi ya mazao yanayovutia magonjwa au wadudu katika bustani yako. Mfano mazao kama mipapai na bamia huvutia nzi wadogo weupe wanaoeneza ugonjwa wa “ukoma wa nyanya”.
Mwisho, tumia madawa ya asili na viwandani ili kupunguza kuenea kwa magonjwa na wadudu.
Kanuni za kukinga magonjwa na wadudu kwa kutumia madawa
Unalazimika kukinga mboga dhidi ya magonjwa na wadudu kwa kutumia madawa ya asili na viwandani pale mbinu nyingine ambazo zimetajwa hapo nyuma zinaposhindwa kuleta mafanikio.
Zifuatazo ni baadhi tu ya kanuni ya kutumia madawa ya asili na viwandani:
- Kwa usalama wa mlaji, unashauriwa kupiga madawa hasa ya viwandani siku 14 kabla ya kuvuna mboga. Pia epuka kupiga madawa mara kwa mara.
- Epuka Kupiga dawa ya aina moja mara kwa mara dhidi ya ugonjwa au mdudu wa aina moja kwani kufanya hivyo huwafanya wadudu kujenga sugu dhidi ya dawa hiyo.
- Epuka kupiga dawa wakati wa upepo mkali au jua kali sana kwani kiasi kikubwa cha dawa kinaweza kupotea hewani. Pia usipige dawa wakati wa mvua (mara tu kabla ya mvua) kwani maji ya mvua yataosha na kupunguza nguvu ya dawa.
- Piga dawa wakati wa asubuhi hasa kukinga magonjwa ya ukungu yapendayo unyevunyevu. Kwa kuzuia wadudu, ni vizuri kupiga dawa wakati wa jioni. Wakati wa jioni dawa huua wadudu zaidi kwani hukaa muda mrefu juu ya majani kabla ya nguvu yake kuharibiwa na jua.
- Weka kiwango cha dawa kama ilivyo elekezwa na watengenezaji au watalaam. Kiasi kidogo cha dawa katika maji hufanya viini vya magonjwa na wadudu kuwa sugu.
- Zingatia kuwa kiasi cha sumu ndani ya kasha au kopo la dawa hutofautiana kati ya kampuni na kampuni iliyotengeneza. Ikiwezekana tafuta ushauri kwa muuza madawa au wataalam waliokaribu nawe.
- Piga dawa ya kutosha sehemu zote za mmea kwani baadhi ya wadudu au magonjwa hukaa na kushambulia sehemu ya chini ya majani.
- Andaa vizuri bomba la kupigia dawa kabla ya kuchanaganya dawa na maji ili dawa iweze kutoka vizu
ri.
- Madawa hutofautiana sana nguvu za kuua wadudu, hivyo changua madawa yanayofaa kufuatana na ugonjwa na wadudu.
Baadhi ya madawa ya asili
Madawa ya asili ni mengi ila bado hayajafanyiwa utafiti wa kutosha. Baadhi ya mimiea inayotoa madawa ya asili ambayo yameshajaribiwa Tanzania ni muarobaini (mbegu na majani), kitunguu swaumu, manung’anung’a, tumbaku, pilipili kali, pareto, n.k. Muarobaini ni miongoni mwa mimea michahce ambayo mpaka sasa imefanyiwa utafiti wa kiina. Mfano, kuchanganya nusu kilo ya mbegu za muarobaini zilizotwangwa katika lita ishirini za maji husaidia kuua wadudu mbalimbali wakiwemo funza wanaotoboa matunda ya nyanya.
Uzuri na Hasara za Madawa ya Asili
Madawa ya asili ni bora zaidi kuliko madawa ya viwandani kwani sumu yake ni kidogo na hupungua haraka baada ya kupiga dawa. Hivyo ni salama zaidi kwa mpigaji dawa na mlaji mboga. Hivyo kupendekezwa katika kilimo hai na hifadhi ya mazingira
Kasoro kubwa katika kutumia madawa ya asili ni kama zifuatayo:
- Hayajafanyiwa utafiti wa kutosha ukilinganisha na yale ya viwandani. Mfano, nitumie dawa ipi inayofaa kwa mdudu yupi?.
- Yanakinga zaidi mboga dhidi ya wadudu waharibifu kuliko magonjwa.
- Uwiano wa kuchanganya dawa na maji bado haujulikani vizuri. Mfano, niweke kiasi gani cha dawa katika kiasi gani cha maji?
- Kwa kuwa nguvu yake ni kidogo, hayatafaa kuzuia mashambulizi makubwa ya magonjwa au wadudu.
Uzuri na kasoro za madawa ya viwandani.
Madawa ya viwandani yana sumu nyingi zaidi na hivyo huzuia haraka zaidi mashambulio ya magonjwa na wadudu. Hivyo, hutumika sana katika kilimo cha mboga na mazao mbali mbali kuliko madawa ya kienyeji. Tatizo la haya madawa ni kwamba ni hatari kwa mkulima, mlaji wa mboga, mazingira na pia gharama zake ni kubwa
Huduma za Kilimo Biashara
- Je unapata changamoto ya kujua dawa zipi zinafaa kwenye magonjwa au wadudu kwenye mazao yako?
- Je shamba lako limekubwa na magonjwa au wadudu na hujui cha kufanya?
- Je ungependa kufahamu gharama zinazohitaji kwenye kilimo cha vitunguu na namna unavyoweza kujua makadirio ya faida utakayoipata?
- Je Ungependa kulima Kilimo cha Uhakika Cha Zao lolote? Hata kama huna elimu ya Kilimo?
- Je unatamani Kulima kilimo biashara cha zao lolote ila hujui uanzie wapi?
- Watu wengi hua wanasikia stori za namna ya kupata faida kubwa kwenye kilimo, lakini wakiingia wanajikuta hawapati matokeo sawa na walivyosikia zile stori/hadhithi. Na wakati mwingine wanapata hasara kabisa. Je unajua kwanini?
Kukabiliana na baadhi ya changamoto hizo hapo juu: Kilimo biashara inakuletea huduma zifuatazo:
Huduma ya Kwanza: Uchambuzi wa Gharama na Faida (Cost benefit Analysis – CBA) wa Zao lolote utakalotaka kulima Kibiashara.
Kwanini CBA? Baadhi ya Manufaa ya kuanza na CBA ni:
- CBA itakusaidia kujua Rasilimali na gharama zinazohitajika kwenye uwekezaji wa kilimo unachotaka kufanya. Hii itakusaidia kufanya maamuzi ya kuendelea na wazo la kulima zao hilo au itakubidi ufanye zao lingine.
- CBA itakusaidia kujua mgawanyiko wa gharama zinazohitajika. Mfano kama kilimo cha vitunguu kinahitaji mtaji wa milioni 2. Haina maana kwamba lazima uwe na hizo milioni mbili ndio uanze kilimo cha Vitunguu. Inaweza kua inahitajika laki 5, halafu baada ya mwezi ikahitajika milioni moja, halafu mwishowe ikahitajika laki 5. Sasa bila kujua mgawanyiko huo unaweza kudhani ni ngumu kufanya kilimo cha vitunguu kwasababu ya mtaji mkubwa unaohitajika, kumbe unaweza kuanza na kiasi fulani. CBA itakupa picha kamili kwenye hilo.
- CBA itakusaidia kujua makadirio ya mavuno na mapato yatakayotokana na Kilimo cha zao unalotaka kufanya. Hakuna mtu anayependa kufanya kitu bila kujua manufaa ya kile anachokifanya. Hivyo CBA itakupa picha ya kile utakachokipata.
Huduma hii inapatikana kwa gharama ndogo ya 20,000/= (Elfu Ishirini tu).
Huduma ya Pili: Master Plan. Huu ni Muongozo au Mpango kazi wa Kilimo cha zao unalotaka kulima kibiashara. Mpangilio huu unakuonyesha shughuli zote za Shambani na muda wake wa kufanyika. Hii itawasaidia wale ambao wanataka kufanya kilimo lakini hawajui kipi kianze na kipi kifuate. Muongozo huu utakuonyesha aina ya mbolea na kiasi kinachohitajika, aina za madawa ya magonjwa na wadudu na kiasi gani cha uchanganyaji wa dawa hizo, Umwagiliaji, na mambo mengine mengi.
Gharama ya kutengnenezewa Mungozo (Master Plan) ni 20,000/= (Elfu Ishirini tu).
Kwa watakaohitaji Huduma zote mbili (Master plan na CBA) watafanyiwa kwa 30,000/= (Elfu thelathini tu)
Huduma ya Tatu: Ushauri wa madawa ya wadudu na magonjwa. Hapa kwanza utasaidiwa kutambua ugonjwa au mdudu aliyeko shambani kwako na dawa za kuudhibiti ugonjwa ua wadudu kikamilifu. Mfano: Mkulima mmoja alinipigia simu, akilalamika amenunua dawa (yeye anaiita sumu) akapiga shambani kwake lakini hakuna matokeo. Katika kumhoji nikagundua shamba lake lilikua na tatizo la ugonjwa, ila yeye alipiga dawa ya wadudu. Akiwa anasubiria matokeo, ugonjwa ukazidi kuenea tu, mwishowe akapoteza mazao na gharama za dawa. Wakulima wengi sana wamekua wakipitia hali kama hiyo, kutokana na kutokua na elimu ya wadudu, magonjwa na madawa, wamejikuta wakichanganya mambo na kushindwa kupata matokeo mazuri. Wakati mwingine baadhi ya wanaouza madawa nao pia wanakua hawana elimu hiyo hivyo kukuuzia dawa yeyote tu, au wengine kwa tama ya fedha anakwambia chukua hata hii inafanyaga kazi, ili mradi usiondoke pale bila kununua.
Katika kupunguza au kuondokana na tatizo hili, Kilimo Biashara tumekuja na huduma ya kumsaidia mkulima kutambua ugonjwa au wadudu walioko shambani kwake. Mkulima anatupigia simu na kutuelezea dalili za ugonjwa au sifa za mdudu aliyeko shambani, kisha wataalamu wetu kutokana na utaalamu na uzoefu wao wataweza kufahamu aina ya mdudu au ugonjwa huo. Kuna wakulima wengine wako kidigitali zaidi, wana simu zenye uwezo wa kupiga picha na kututumia picha za mimea au wadudu kupitia whatsapp au email, njia hii imekua ikirahisisha sana utambuzi wa magonjwa au wadudu. Baada ya utambuzi wa ugonjwa au wadudu, mkulima anashauriwa dawa aina mbili au tatu zenye ufanisi katika kudhibti ugonjwa au wadudu husika. Pia mkulima ataelekezwa kiasi cha uchanganyaji na maji na upigaji wa dawa husika.
Kupata Huduma hii ni shilingi 10,000/= (elfu kumi) tu.
Kwa ushauri, maulizo au kupata huduma zetu waweza kuwasiliana nasi kupitia namba ya simu 0763 071007, au waweza kutuandikia email kupitia: ushauri@kilimo.net
No comments.