KILIMO CHA MATIKITI MAJI KIBIASHARA
Tikiti maji ni zao linalolimwa kibiashara.hufahamika kama Watermelon, na kwa jina la kibotania (Botanical name) hujulikana kama Citrullus lanatus. Ni moja ya mazao yanayotoka kwenye familia ya mimea ya Cucurbitaceae, mazao mengine ynayotoka family hiyo mojana tikiti maji, ni matango (Cucumber), maboga (pumpkin), musk melon, squash n.k. Inaaminika kwamba asili ya tikiti maji ni huko jangwa la Kalari ambako lilikua linapendwa sana kwa sababu lilitumika kupooza koo au kukata kiu kwa watu wanaoishi karibu na Jangwa la Kalahari hii ni kwasababu tikiti maji ni tunda lenye maji mengi. Inakadiriwa zaidi ya asilimia 90 ya runda la tikiti ni maji, ndio maana huitwa tikiti maji. Hata hapa Tanzania Tikiti maji soko lake zuri ni kipindi cha joto ambako walaji wengi hutumia kwa ajili ya kukata kiu kutokana na joto. Wauzaji wa matikiti katika masoko mabalimbali wanasema biashara ya tikiti ni nzuri sana wakati wa kiangazi/joto na wakati wa baridi biashara hiyo inadorora. Taarifa kama hizo ni nzuri sana kwa mkulima mjasiriamali anayelenga uhitaji wa soko.MAANDALIZI YA SHAMBA:
Shamba la kupanda matikiti maji linapaswa liandaliwe vizuri, udongo ulainike vizuri usiwe na mabonge ya udongo kwa maana mbegu za tikiti zinapdwa moja kwa moja shambani (direct seeding) na mbegu hizo zina umbo dogo, hivyo zinahitaji udongo uliolainika vizuri ili kuweza kuota. Shamba linapaswa kua sehemu ambayo hakuna miti, maana kivuli cha miti kinaweza kusababisha matikiti yasitoe matunda.
.
Vifuatavyo ni Vigezo vya kuzingatia wakati wa kutafuta shamba/eneo la kupanda matikiti maji.
- Aina ya Udongo
Tikiti maji linaweza kulimwa katika aina nyingi za Udongo, lakini yanafanya vizuri zaidi kwenye udongo kichanga (fine sand), tifutifu na tifutifu kichanga. Aina ya udongo itaadhiri uzalishaji wa tikiti kutegemeana na hali ya hewa. Kwa mfano unapolima tikiti kwenye udongo wa mfinyazi wakati kuna mvua nyingi, mimea ya matikiti haitaweza kustawi, kwa sababu udongo wa mfinyazi utatuamisha maji kwasababu ya mvua na hivyo mimea itakufa. Vilevile unapootesha matikiti kwenye udongo wa kichanga, halafu pawe hakuna maji ya kutosha mimea itakufa kwa kukosa maji. Pia kumbuka udongo wa kichanga unapoteza maji kwa haraka, hivyo unapolima kwenye udongo wa aina hiyo hakikisha una maji ya kutosha na umwagiliaji uwe wa mara kwa mara.
- Utoaji wa maji shambani (Drainage).
Kigezo kingine ambacho mkulima anapaswa kuzingatia wakati wa kutafuta eneo la kupanda matikiti ni Udongo wenye uwezo wa kutoa maji, yaani udongo usiotuamisha maji. Unaweza kutengeneza mifereji itakayoasaidia kuondoa maji yanayozidi shambani.
- Mteremko wa Ardhi (Topography)
Ni ile hali shamba linapokua limeinuka upande mmoja na upande mwingine kuna mteremko au unaweza kuiita slope. Shamba lenye mteremko au slope ni rahisi sana kukumbwa na mmomonyoko wa udongo ambao utaharibu mimea yako. Hakikisha unapoachagua shamba, basi unaepuka maeneo ya mtindo huo.
- Mwanga wa jua (Sunshine).
Katika upandaji wa zao lolote mwanga wa jua ni muhimu sana kwasababu husaidia kwenye utengenezaji wa chakula cha mmea (Photosynthesis). Kwa upande wa matikiti, mwanga wa jua una athari kubwa sana kwenye mazao, aidha kupungua au kuongezeka. Mmea wa Tikiti unahitaji angalau masaa 6 ya mwanga wa jua. Hii inasaidia sana katika utengenezaji wa sukari kwenye tikiti. Pia mwanga wa jua husaidia ukuaji wenye afya wa mmea wa tikiti. Hivyo kwa ukuaji mzuri, unapochagua eneo la kulima tikiti chagua eneo ambalo Mimea itapata mwanga wa jua wa moja kwa moja (direct sunlight) kwa angalau masaa 6 hadi 8 kwa siku. Hii ikimaanisha kwamba eneo liwe mbali na majenngo au miti mikubwa inayoweza kuleta kivuli kwenye shamba.
Madhara ya Kukosa Mwanga wa Kutosha
Matikiti yaliyopo eneo lenye mawingu ya mara kwa mara au eneo mbalo halipati mwanga wa jua wa kutosha, huzaa matunda yenye ladha mbaya.
Mimea ikikosa mwanga, hunyauka na kufa.
Uchavushaji (pollination) kwenye Mimea ya Matikiti hufanywa na wadudu kama nyuki, Shughuli za nyuki zinapungua wakati wa baridi au wakati wa mvua kwa sababu vipindi hivyo hakuna mwanga wa jua wakutosha. Hii ina maana kwamba hata eneo lenye kivuli sio rafiki kwa shughuli za uchavushaji
Matikiti yanahitaji joto ili kuzalisha matunda matamu. Hii ikimaanisha kama eneo litakua lina kivuli halitakua na joto hivyo matunda yatakosa sukari
- Maji
Upatikanaji wa maji katika eneo la kuzalishia matikiti ni kigezo kingine muhimu cha kuzingatia wakati wa kuchagua eneo. Ili kufanya kilimo chenye uhakika, jitahidi eneo lako liwe karibu na chanzo cha maji cha uhakika, kwa ajili yakufanya umwagiliaji.
- Kufikika.
Eneo liwe sehemu kunakofikika hususani. kwa miundombinu ya barabara. Eneo liwe mahali ambapo gari kubwa inaweza kufika, ili kusaidia usafirishaji wakati wa kuvuna.
AINA ZA MBEGU NA UCHAGUZI WA MBEGU NZURI
Uchaguzi wa aina ya mbegu (variety) ni kitu cha msingi sana katika kilimo cha tikiti ambapo shughuli zote zinajengwa kwenye msingi huo. Hii kimaanisha kama ukikosea kuchagua aina ya mbegu nzuri hata ukijitahidi mbinu nyingine, hazitakua na tija. Kuchagua mbegu nzuri na zenye ubora sio kazi nyepesi, ni ngumu kweli kweli, kwa bahati mbaya wakulima wengi hukimbilia zile mbegu maarufu ambazo zinatangazwa zaidi, ambapo mara nyingi wanapokwenda kwenye uhalisia kwa kulima mbegu hizo hukumbana na hali tofauti na waliyoisikia kwenye matangazo.
Vigezo vya muhumu kuzingatia wakati wa Kuchagua Aina ya Mbegu:
Kabala mkulima hajafanya maamuzi ya mbegu ipi alime, ni vyema akazingatia vigezo vifuatavyo:
Ni aina ipi ambayo ina soko? Kama unalima kibiashara, hichi ni kigezo cha kwanza kuzingatia, tambua kwanza soko unalolenga linapendelea aina ipi ya matikiti. Kwa mfano kwa kanda ya ziwa, matikiti yenye mistari ya Zebra, hayana mpenyo kwenye soko la kanda ya ziwa, walaji wengi bado wanapendelea yale matikiti ya kijani au wengine wanayaita meusi, yasiyokua na mistari au mabakamabaka. Sasa kwa kusikia maeneo mengine kama Arusha na kwingine kwamba watu wanalima matikiti ya mistari ya zebra na Wewe uko kanda ya ziwa , halafu ukaingia kulima hayo ya Zebra wakati soko lako unalolenga ni Mwanza, lazima wakati wa kuuza utalalamika hakuna soko. Hivyo ni muhimu kufahamu soko lako kwanza, jua linahitaji aina ipi kisha ndio ufanye uamuzi wa kulima aina ipi.
Uwezo wa kumudu au kukubali mazingira utakayolimia (adaptability). Sio aina zote za matikiti zinakubali kila aina ya mazingira, kuna maeneo ambayo aina fulani inakubali, na ila aina nyingine ikagoma. Hivyo fahamu uwezo wa aina hiyo ya tikiti kuota kwenye mazingira yako. Kama kuna majirani wanaolima matikiti au watu wa maeneo ya karibu na mazingira yako wanalima tikiti, unaweza kufanya utafiti wako kwa kujua ni aina ipi inafanya vizuri kwa hao majirani zako.
Angalia gharama za kuhudumia/matunzo.Kuna aina za tikiti zinahitaji matunzo ya gharama kubwa kama vile mbolea za kutosha, madawa n.k. Hivyo ni muhimu kujua gharama zake kabla hujanunua, ili kama uwezo wako hautamudu, uchague aina nyingine, ili usije pata hasara kwa kuchukua aina yenye kuhitaji matunzo makubwa ukashindwa kuyahudumia
UPANDAJI
Katika upandaji wa tikikiti zipo aina nyingi za upandaji, ila kwa hapa tutagusia aina mbili ambazo zina matokeo mazuri:
Upandaji wa Mstari mmoja (Single row system). Hapa tuta linakua na mstari mmoja tu wa tikiti. Nafasi ya mstari hadi mstari ni mita 2 au mita mbili na nusu (2 – 2.5m). Nafasi ya mche hadi mche ni sentimita 60.
Upandaji wa Mistari miwili (double row system).Hapa tuta linakua na mistari miwili ya tikiti. Nafasi ya mstari hadi mstari ni mita tatu na nusu hadi mita nne (3.5- 4.0m). Nafasi ya mche hadi mche ni sentimita sitini (60cm).
Kwenye shimo moja zinapandwa mbegu mbili, kama zikiota zote mbili, basi moja unaingoa na kuhamishia kwingine ambako kunaweza kua ni sehemu mpya kabisa au ni hapohapo shambani, kwenye shimo ambalo hazijatoata au ziliota zikafa.
UWEKAJI WA MBOLEA
Mbolea ya Samadi: Weka shamba lako mbolea ya samadi iliyokauka vizuri. Kiasi kinachotosha ni tani 5 had 8 kwa ekari moja.
Mbolea za kupandia: Mbolea ya kupandia unaweza kutumia DAP, Minjingu au mbolea yeyote yenye kirutubisho kikubwa cha Phosphorous. Mbolea ya Kupandia inawekwa wakati wa kupanda, kwenye shimo la kupandia, unatanguliza mbolea ya kupandia wastani wa gramu 5, kisha unafunika na udongo kidogo kisha ndio mbegu ya tikiti inafuata. Lengo hapa ni mbegu isigusane na mbolea ya kupandia.
Mbolea za Kukuzia: Mbolea za kukuzia ni zinazotumika sana kwenye kilimo cha tikiti ni kama NPK, na CAN.
Mbolea za Majani (foliar fertilizers). Hizi ni mbolea zinazowekwa kwenye majani kama unavyopulizia dawa (spraying). Mbolea hizi hua ni zile zenye vile virutubisho vinavyohitajika kwa kiwango kidogo (micronutrients). Unapiga mara matikti yanapoota, kisha unapiga tena wakati wa utoaji wa maua, halafu unamalizia na wakati wa utengenezji wa matunda.
MAGUGU NA PALIZI
Magugu yana madhara kwa zao lolote, ila yana madhara makubwa zaidi kwa zao la tikiti maji. Lakini ni muhimu kufahamu kwamba Udhibiti wa magugu au palizi kwenye matikiti kunahitaji umakini sana kwa maana tikiti hazihitaji kubugudhiwa au kuguswaguswa/kutingishwatingishwa maana husababisha mmea mzima kupata stress kitu ambacho kitaathiri mpangilio wa uzalishaji. Palizi pia inaweza kuharibu maua au matunda yale madogo yaliyoanza kutengenezwa.
ATHARI ZA MAGUGU KWENYE UZALISHAJI WA MATIKITI MAJI
Magugu yanashindania virutubisho na mazao (compete with plant for nutrients). Na magugu yana uwezo mkubwa wa kutumia virutubisho kuliko mazao, ndio maana magugu yanakua kwa haraka kuliko mazao yaliyopo shambani. Hii hupelekea uzalishaji wa tikiti kupungua.
Magugu yanashindania maji na mazao ya tikiti, na kupelekea tikiti kukauka. Kama ilivyo kwa virutubisho hivyohivyo magugu yana uwezo wa kutumia maji haraka kuliko mazao.
Magugu yanapunguza utoaji wa maua kwenye tikiti kutokana na kupungua kwa mwanga wa jua. Magugu husababisha kivuli kwa matikiti hivyo kukosa mwanga wa kutosha ambao husaidia mimea kutoa maua.
Magugu pia yanapunguza utoaji wa matunda kwenye mmea. Maua yakiwa machache hasa maua ya kike ina maana matunda yatakayotengnezwa yatakua machache zaidi.
Magugu yanazuia shughuli ya uchavushaji (pollination) shaghuli ambayo ni muhimu sana kwenye kilimo cha matikiti. Hii ina maana wadudu wanaofanya ushavushaji kama Nyuki, watakimbilia kwenye maua ya magugu na kuacha kushughulika na maua yamatikiti.
Magugu pia yanavutia wadudu na magonjwa kwenye mazao
UTHIBITI WA MAGUGU
Mpaka wa sasa hakuna madawa chaguzi (selective herbicides) ya kufanya palizi kwenye tikiti. Madawa chaguzi, ni yale madawa ambayo unapiga shambani alafu yanaua magugu lakini hayana madhara kwa mazao. Mfano dawa yenye kiambato (active ingredient) cha Oxyfluorfen ya kupiga kwenye vitunguu, inapopigwa kwenye shamba la vitunguu, inaangamiza magugu lakini vitunguu vinabaki salama. Kwa upande wa zao la tikiti bado hakuna dawa za namna hiyo.
Hivyo magugu kwenye tikiti yanahitahitji kufanyiwa palizi kwa mkono au jembe wakati mimea ikiwa midogo. Epuka kufanya palizi wakati tikiti limeshaanza kutoa maua.
Kama umefanya palizi mapema na bado kipindi cha utoaji maua pakawa na mgugu basi subiri kidogo, kipindi cha utoaji maua kikiisha tu, basi ng oa hayo magugu kwa mkono, huku ukiepuka kugusagusa mimea ya tikiti.
Uwekaji wa Matandazo (Mulching)
Njianyingine ya kudhibiti magugu ni njia ya kuweka matandazo (mulching). Kuna ana mbili za matandazo, ambayo ni matandazo ya Asili (orgnic Mulch) na Matandazo yasiyo ya asili (inorganic mulch).
Uwekaji wa matandazo ya asili (Organic mulching)
Mbegu chotara (Hybrid) ya tikiti maji
Huzaa matunda 2 hadi 3 kwa mmea mmoja.
Matunda yake huwa na uzito kilo 8 hadi 10.
Ndani ni rangi ya nyekundu iliyokolea, ni tamu, sukari yke ni 12%
Hukomaa kwa siku 70 hadi 80
Hufaa kusafirisha kwenda masoko ya mbali bila kuharibika.Mahitaji ya mbegu kwa ekari 1 ni: gram 500
1. Mwongozo wa kilimo biashara cha Vitunguu maji
2. Mwongozo wa Kilimo cha TIkiti maji
3. Mwongozo wa Kilimo cha NyanyaVitabu vyote hivi 3 unavitapata kwa 20,000 tu badala ya 45,000.
Namna ya Kupata nakala zako:
Vitabu hivi vinapatikana kwa njia ya mtandao (email, telegram, au Whatsapp) Yaani unatumiwa kwenye email au whatsapp.
Unafanya malipo ya 20,000 Kwa mpesa 0763 071007 au Tigo pesa 0712578307 (Jina Litaonyesha Daudi Mwakalinga)
Ukishafanya malipo unatuma Ujumbe wenye Jina na email yako kwenda 0763 071007 au 0712 578307.
Kama huna email na ungependa kutumiwa Kitabu kwa Whatsapp basi utatuma ujumbe WhatsApp kwenda namba 0763 071007. VItabu utavipata ndani ya dakika 5 hadi 10 baada ya kufanya malipo.
Wahi Ujipatie nakala zako kwa bei ya OFA. Mwisho wa OFa ni 8.07.2018
Ni mimi Mtaalamu wako Daudi Mwakalinga (0763 071007). Tukutane wakati mwingine.Karibu sana
- Asante na Karibu sana.
- www.kilimo.net
- Kama ulikua hujasoma makala ya Kilimo cha Vitunguu basi bonyeza hapa:Lima Vitunguu Kijanja.
Response to "KILIMO CHA MATIKITI MAJI KIBIASHARA"
Thanks mzee kwa elimu
Asante sana Kaka Justine. Kujifunza zaidi Endelea kutembelea blog yetu ya http://www.kilimo.net
Asante mkuu kwa elimu mujarabu. Samahani, nimepanda matikiti kwenye vifuko vya saruji ili kudhibiti upotevu wa maji na magugu. Je, ni njia sahihi?
Katika kupanda nimechanganya mbolea ya samadi ya nguruwe kwa uwiano wa 1:4 yaani kwa kila mabakuli manne ya udongo nimeweka mbolea bakuli moja. Je, ni uwiano sahihi?
Matumizi ya samadi pekee badala ya mbolea za madukani yataweza kunipa matokeo bora?
Ninaomba hayo majibu angalau kwa kuanza tafadhali
Mdau sasa hiyo mbolea ya nguruwe inakuwaje kwa waislam…Hii hauwezi kuwa baadae utalisha waislam tikiti pork?
Habari Daniel
Asante kwa Maswali yako mazuri. Kwanza nikupongeze kwa ubunifu wako wa kutumia vifuko vya saruji katika kutatua hiyo changamoto ya maji. Hiyo ni sawa kama inafanya kazi vizuri.
Kuhusu Mbolea nayo haina shida, mchanganyo huo ni sawa pia. Ila kwenye kutumia mbolea ya samadi peke yake haitakupa matoke mazuri. Kwanza samadi haina virutubisho vyote na kwa wingi unaohitajika. Mfano huwezi kujua hiyo samadi ya nguruwe ina Nitrogen kiasi gani, Potassium au Phosphorous kiasi gani n.k Mmea wa tikiti unavyokua katika hatua za ukuaji unahitaji virutubisho vya aina mbalimbali. Mfano, kipindi cha maua na kutengeneza matunda inahitaji mbolea zenye Potassium na Calcium. Ambapo utatumia CAN au MOP. Hiyo Huduma ya Master Plan tunayotoa, inatoa maelekezo ya mbolea zote zinazohitajika kuanzia kupanda hadi kuvuna. Kwa maelezo zaidi waweza kuwasailiana nasi kwa namba 0763 071007
mi ninazo heka mbili kwa sasa zina wiki tatu chini, ila nategemea kujifunza mengi na kama yupo anayefahamu soko zuri au wanunuzi kanda ya ziwa naomba aniunganishe nao 0755475282. Ni mkulima mdogo bado lakini ndo naelekea ivyo.
Nashukuru Sana kwa makala yenu nzuri kuhusu kilimo cha tikiti. Nimekuwa na idea ya kulima zao hili kwa muda mrefu ila sikuweza kujua kuwa naanzia wapi na ntaishia wapi. Lakini baada ya kusoma makala hii nmejikuta naweza kufanya mambo makubwa sana. Nitawatafuta ili mnipe msaada wa kitaalamu zaidi ili niwekeze kwenye zao hili linalopendwa kuliwa na watu wengi kwa sasa .
Thank you so very much bros.
Asante kwa makala nzuri…ningependa kuuliza he haiwezekan kuanza na mtaji wa chin ya milioni mbili?
Naomba aliye na farmguard anipatie kopo 20
ahsanten sana kwa kutoa utajili kwa wenye akili timamu,naomben kuuliza kwa mfano unataka kuanza kilimo cha tikiti inagharim kama shingap mpaka kutoa mzigo shambani?
shukria saana!
Ndugu David Nashukuru sana kwa mchango wa elimu yako mtandaoni, mwakajana nililima matikiti lakini nilikula hasara, pamoja na hayo sikukata tamaa changamoto ni mtaji, Maana najikuta Nabaki na mikakati kibao bila kufanya chochote kisa mtaji, je! Nifanyeje?
Asanteni sana kwa makala yenu nzuri mm nimeamasika nifanyeje ili nifanikiweľ
Kweli nimebarikiwa na kufarijika sana kwa elimu hii nzuri. Nimekuwa nikitamani kwa muda mrefu kulima tikiti,lkn shida ilikuwa ni wapi pa kuanzia maana sikuwa na elimu nzuri ya kilimo hiki. Naamini huu ni mwanzo mzuri na muda si mrefu ntaenda kukamilisha hitaji la moyo wangu. Nashukuru sana kwa makala hii japo bado nahitaji kuendelea kujifunza zaidi kutoka kwenu.
NINA SHAMABA LA MATIKITI LINALO TEGEMEWA KUVUNWA TANI 5 KATIKATI YA MWEZI WA 3. NAOMBA USHAURI WA SOKO ZURI LA MATIKITI
Nashkuru kwa somo zuri.
Naskia viwandani kuna bei nzuri sana…..usha fuatilia hili?
Natafuta soko la sugar queen water melon,nitavuna may wiki ya pili 2018.nahitaji vitabu vyako.nipo mza.
Nashukuru sana ndugu Daudi kwa elimu hii muhimu, mimi ninashamba langu nililoandaa kwajili ya kilimo cha matikiti lakini kwa kukosa elimu ya kuridhisha nikaamua kupanda mahindi na chia seed lakini sasa naanza upya mungu akubariki sana.
Nahitaji vitabu hivi vyote ASAP.
Nashukuru kwa somo zuri hivi heka moja inaweza ikagharimu shilling ngapiiiii
Safi kk!!!! Ila iki kilimo bado kwangu ni changamoto ni soko km Kuna mtu mwnye soko zuri anichek kwenye namb Zang 0715117702 au 0692179291
Nauliza kuusu kilimo cha matikiti ,tikiti tangu zipandwe zinaota baada ya Siku ngapi?