KANUNI ZA UPANDAJI MBOGA NA MATUNDA

KANUNI ZA UPANDAJI MBOGA NA MATUNDA

Utangulizi

Upandaji mboga na matunda katika maeneo mengi ya nchi yetu unazidi kukua siku hadi siku. Bidhaa au mazao yanayopatikana katika sehemu hizi huuzwa katika masoko ya humu nchini na mengine soko la nje. Ni muhimu kutaja hapa kwamba wanunuzi na walaji wa mazao na bidhaa zinazotokana na mazao haya wanazidi kuwa waangalifu na huzingatia ubora wa mazao wanayopata kutoka kwa soko. Kwa sababu hii basi, mkulima anapaswa kuzingatia kanuni zifuatazo:

Mimea ya kukuza

Ni muhimu kwa mkulima kujiuliza je, katika msimu huu ni mmea gani ninastahili kupanda? Bila shaka mkulima anapaswa kufanya uamuzi kuhusu mmea au mimea atakayopanda na kukuza. Ni sharti basi mkulima afanye makadirio ya gharama za mimea anayotarajia kupanda na kutambua faida kutokana na mimea hii mbalimbali.

Akishatambua ni mimea gani anapanda na kukuza ni muhimu pia kuangalia mambo yafuatayo:

• Aina gani au ni shina mama lipi litakalotumika wakati wa kupanda

• Ubora wa mbegu

• Kinga dhidi ya wadudu na magonjwa

Wakati wa kupanda

Kwa mkulima anayechukulia kilimo kama biashara, ni muhimu ajiulize je, ni wakati gani wa kupanda? Kwa wakulima wengi jawabu linalokuja kwa fikra zetu mara moja ni wakati wa mvua. La hasha! Wakati mzuri wa kupanda unatambulika vyema tunapozingatia mambo fulani katika soko kama vile:

• Ni wakati au muda gani mmea wako utakomaa?

• Wakati uhitaji (demand) wa zao uko juu.

• Wakati bei ya mazao ni nzuri kwa mkulima.

• Wakati utoaji (supply) wa zao uko chini kabisa.

Ni muhimu kwa mkulima kuwa na muongozo wa upandaji akitilia maana uhitaji na ugavi wa mazao sokoni.

Mahali kwa kukuza

Mimea inapopandwa mahali au maeneo yanayokubaliana nayo basi mazao huwa mazuri zaidi. Ni muhimu basi kwamba historia ya eneo ambalo mmea unatarajiwa kukuzwa ijulikane kikamilifu. Historia itapatikana kutokana na kuchunguza, majadiliano au kusoma taarifa kuhusu eneo hili. Habari hizi sharti zigusie mimea iliyokuzwa hapo awali, magonjwa na wadudu wanaopatikana hapo, aina gani za mbolea zilitumika hapo na kadhalika.

Ni muhimu kufahamu kwamba kila mmea una mahitaji tofauti kwa kukua vyema.

Mkulima ni lazima azingatie haya:

1. Udongo: Udongo wa eneo hilo ni sharti ufanyiwe utafiti na kufahamika wazi aina, upungufu wake, na sifa zake muhimu.

2. Mvua: Mvua inayopatikana katika eneo hili ni muhimu kujulikana, kama ni viwango vyakutosha au la.

3. Joto: Mimea ni lazima ikuzwe katika maeneo yenye joto kulingana na mahitaji ya mmea.

Upanzi na ukuzaji: Katika kilimo cha biashara ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:

Utayarishaji shamba: Shamba ni sharti zitayarishwe ipasavyo kwa kuchimbua kikamilifu, kuondoa kwekwe na kuvuna mchanga. Kwa kuboresha mazao na wingi wake, ni muhimu mkulima atumie mbinu zilizo na gharama ya chini lakini apate faida kubwa.

Basi mkulima inapaswa awe na utaalamu wa kilimo katika mambo yafuatayo:

• Uchaguzi wa mbegu

• Upanzi – kutumia mbegu, kupitia kwa nasari (kukuza miche kwenye kitalu)

• Kutoa kwa nasari/Kitaluni hadi shambani

• Uwekaji mbolea

• Unyunyizaji maji (umwagiliaji)

• Kuthibiti wadudu na magonjwa

• Kukomaa kwa matunda na mboga

• Uvunaji mazao

• Utayarishaji wa mazao kwa mauzo ama kuhifadhi

• Mauzo

Wateja

Wateja wa kisasa hujali sana ubora wa mazao na afya zao. Ni muhimu kwa mkulima kutambua mahitaji na matakwa ya wateja wake kabla ya kupanda na kutunza mimea yoyote.

Hapa chini nimekuwekea jedwali lenye kuonyesha Miezi sahihi ya Kupanda (baadhi ya mazao ya mboga) ili kukutana na bei nzuri sokoni

GoodNews

Habari njema ni kwamba Vitabu vya Tikiti Maji sasa vimetoka tena
Jipatie Nakala yako sasa kwa Ofa ya nusu bei ya 10,000 tu badala ya 20,000. Kitabu kinakufikia popote ulipo. Ni hakika kwamba utajifunza mambo muhimu sana na ya faida kwenye kitabu hiki.

OFa hii mwisho 15.12.2019

Mawasiliano:
Simu: 0763071007
Email: ushauri@kilimo.net

Jipatie OFa ya Miche ya Matunda hapa: https://kilimo.net/2019/11/28/ofa-ofa-ofa-miche-ya-matunda/

Kwa ushauri kuhusu kilimo biashara waweza wasiliana nasi kupitia:
Email: ushauri@kilimo.net
Simu: 0763 071007

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *