Faida za Kilimo cha Miembe (Milioni 8 kwa ekari 1 tu)

Faida za Kilimo cha Miembe (Milioni 8 kwa ekari 1 tu)

Embe ni tunda maarufu na limekuwa likitambulika kama mfalme wa matunda.

Matunda ya embe yanatumika yakiwa mabichi au yameiva. Matunda yaliyoiva yanaliwa kama tunda au pia yanaweza kutengenezwa juisi na jam.
Embe mbichi hutumika katika kutengeneza achali.

Kama ilivyo kwa miparachichi, miembe hukua haraka na haipukutishi majani na hivyo ni mti unaobadilisha mazingira ya mashamba na kuleta hali ya ukijani kwa mwaka mzima.

Miti ya miembe ikipandwa kwa mpango mzuri mashambani inasaidia kurekebisha hali ya hewa kwa kupunguza joto, kuvuta mawingu ya mvua, kupunguza kasi ya upepo, kupunguza mmomonyoko wa ardhi na
kufyonza hewa ya ukaa.

Hivyo Miembe nayo ni miti mizuri kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Miti hii ikipandwa mashambani kwa mpangilio mzuri wakulima wataweza kulima mazao menginena hivyo kujipatia fedha zaidi, matunda na hata kuni.

Miembe hustawi sehemu zenye joto la wastani na lenye maji au mvua za kutosha, hata hivyo miembe haistawi vizuri katika maeneo yeney baridi kali na mvua nyingi kwa mwaka kwa kuwa inahitaji kipindi cha ukame cha miezi isiyopungua miwili hadi mitatu ili kuwezesha kutoa maua. Pia miembe hihutaji udongo wenye kina usio twamisha maji na usio na chumvi chumvi.

Aina za maembe

Zipo aina nyingi za embe, kama vile Apple, Ngowe, Boribo, Tommy Atkin, Haden, Van Dyke, Sensation, Alphonso, Sabre, Keit, Kent, Peach. Haya ndiyo maembe yenye soko bora na yanatumiwa kuunganishwa/kubebeshwa (Grafting).

MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI

Ili kupata mazao bora ni muhimu kuzingatia kanuni bora za kilimo cha maembe hasa kanuni zifuatazo:

1. Kuchagua aina bora

• Chagua aina bora ya kupanda kulingana na mahitaji ya soko.

2. Kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu

• Fanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara ili uweze

• kudhibiti wadudu na magonjwa ya matunda kabla madhara hayajawa makubwa

• Ni muhimu kudhibiti wadudu, magonjwa na magugu ili kupata mazao bora ambayo yatapata soko zuri na kuweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu.

• Hakikisha shamba ni safi wakati wote ili kupata matunda bora na kurahisisha uvunaji.

Matunzo
• Wakati wa mwaka wa kwanza mche unaposhika kwa shamba ni vyema kuweka kivuli kama ile ya nasari. Pia inasaidia kuweka samadi ili kuhifadhi unyevu wakati wa kiangazi. Usisahau kupatia miche yako maji ya kutosha.
• Changanya mazao kama kunde, maharagwe kati ya mistari ili ardhi itumike ipasavyo.
• Eneo linalozunguka mwembe kama mita moja (1 meter) lisipandwe mimea ili lisidhuru mti wa miembe.
• Ondoa maua yanayotaka mwanzo baada ya kupandikiza.

Kuota matawi (pruning)
Hii inafanywa ili mti upate mwelekeo uliyo bora wa wakati mti utakua umekomaa. Ruhusu mti upate tagaa tatu hadi nne (3-4) zinazoelekea pande tofauti mita moja (1 meter) kutoka chini na zile tagaa zipeane nafasi.
Mara kwa mara mti unapokuwa na tagaa ambazo ni gonjwa, zimekufa na zinazokingana zahitajika kutolewa. Ili kuwe na hewa ya kutosha katikati ya matawi.

Kuvuna
• Miche iliyouzwa au kubebeshwa huzaa kuanzia miaka ya tatu ama nne
• Mwembe mmoja hutoa mtunda 400 – 800 kwa mwaka

Mapato:
Tuangazie makadirio ya Mapato ya Embe.
Ekari 1- inaingia miembe 80 hadi 100 kutegemea na nafasi (Spacing) iliyotumika.
Tufanye makadirio ya mimea 70 tu ndio iliyofanikiwa kukua na kutoa matunda
Mti mmoja wa mwembe hutoa matunda 400 hadi 800 kwa mwaka/msimu. Tuchukue kadirio la chini kabisa la matunda 400

Hivyo Ekari 1= 70 (miti) X 400 (matunda)= 28,000 (matunda)
Bei ya kuuzia shambani ni 300 hadi 600 kwa embe. kutegemea na aina ya embe na ukubwa wa tunda. Tuchukulie kadirio la chini kabisa la 300 kwa embe.

Ekari 1: matunda 28,000 X 300 = 8,400,000 (milioni 8 na laki 4)

Hichi ni Kipato cha uhakika kwa kila mwaka,ukiwa na ekari 1 tu. Sasa fanya uwe na ekari 5 hadi 10.
Pia kilimo cha Embe hakihitaji ufuatiliaji/usimamizi wa karibu sana kama ilivyo mazao ya mboga na matunda. Unaweza kuwa busy na shughuli zako nyingine na bado ukamudu kufanya kilimo hichi cha embe bila stress kabisa na ukawa unaingiza kipato chako kizuri tu.

Hivyo hichi ni kilimo sahihi kwa wale ambao wanapenda kufanya kilimo lakini wamebanwa na majukumu mengine.

Kwa ushauri kuhusu kilimo biashara waweza wasiliana nasi kupitia 0763 071007.

Miche bora ya Miembe

Karibu sana ujipatie miche ya kisasa ya miembe mifupi. Miche hii ni ile iliyobebeshwa (iliyofanyiwa Grafting) hivyo ina wahi kuzaa na mavuno ni mengi zaidi.
Aina tulizo nazo ni Embe Apple, Dodo, Bolibo, Red Indian, Alfonso, nk

Pamoja na Miche utapatiwa ushauri wa kitaalamu.

Vitalu vyetu vya miche vinapatikana Dar na Morogoro. Kwa Dar, tupo hapa Ubungo Mawasiliano., Mlimani City na Mabwepande. Pia tunafanya delivery, kwa wakazi wa Dar, (kuanzia miche 50 tunakuletea kwa gharama nafuu kabisa). Kwa wateja wa mikoani tunatuma, na miche inafika salama kabisa.
Mawasiliano: Simu 0763 071007
Email: ushauri@kilimo.net
Website: www.kilimo.net

Response to "Faida za Kilimo cha Miembe (Milioni 8 kwa ekari 1 tu)"

 • Nina shamba Songwe-napataje mbegu ya muda mfupi na yenye soko-(embe zenye soko),pia nataka kupanda Korosho

 • 1. Nawashukuru kwa Elimu hii muhimu mnayotupa…. ni Mchango mkubwa kwa Maendeleo ya Kilimo na hivyo Uchumi wa Nchi yetu.
  2. Ila je, Mche hadi Mche ni umbali gani? Mimi nataka kupanda Miembe hiyo, Miwili au Mitatu, uani kwangu nina nafasi katika Bustani ya Nyumbani…!

  Wasalaam,

  Saidi Nguba.
  (Simu: 0754 – 388418).
  Ununio, Dar es Salaam.

 • Habari nina miembe hekarimoja na uchee,mwezi wa 12 tunakula mengi yana ishia kudondoka na kuoza natafuta soko kwa mawasiliano 0714005166

 • sawa kuhusu eliku yenu ya Kilimo bora cha Miembe bei ya mche moja ni chilingi ngapi kama nataka miche kumi

 • sawa kuhusu elimu yenu ya Kilimo bora cha Miembe bei ya mche moja ni chilingi ngapi kama nataka miche kumi

 • Leave a Reply

  Your email address will not be published. Required fields are marked *