Faida za Greenhouse

Faida za Greenhouse

Greenhouse(Banda Kitalu):ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu.Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa. Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.
Faida au fursa za Greenhouse

  1. Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi, ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.
  2. Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya uharibifu wa mazao.
  3. Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
  4. Uwezo wa kupata soko zuri la mazao. Greenhouse itakuwezesha kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu,ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei nzuri
  5. Ufanisi katika utumaji wa dawa (viwatilifu) katika kudhibiti wadudu na magonjwa.
  6. Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti wake ni rahisi. Miundombinu ya umwagiliaji inayotumika hapa ni umwagiliaji wa matone (drip irrigation) ambapo maji yanakwenda pale penye mmea tu.
  7. Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili ya kuzoea mazingira ya nje kwanza.
  8. Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (soilless culture).Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuziwa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea

Jipatie Greenhouse au Nethouse za bei nafuu.
Ukubwa wa Greenhouse na bei zake:
Mita 6 kwa 12 Milioni 4.2
Mita 6 kwa 24 Milioni 6.2M
Mita 8 kwa 15 Milioni 5.5
Mita 8 kwa 30 Milioni 12.5
Mita 16 kwa 30 -Milioni 17
NET HOUSE Hizi zinafaa sana kwa yale maeneo ya joto.
Mita 6 kwa 12- Milioni 3.9
Mita 8 kwa 15 Milioni 5.0
Mita 8 kwa 30- Milioni 11
Mita 16 kwa 30 Milioni 15
NB: Tutakufungia Ukubwa wowote unaotaka kulingana na bajeti yako
Package inakuwa Na vitu vifuatavyo:
Utapewa Elimu Kwanza ya Kutosha Greenhouse/ Net House na Drip Irrigation
-Kujengewa greenhouse / Net house Kwa kutumia Miti Imara ya Miti, inayodumu Kwa Miaka kuanzia 15.
Kufungiwa vifaa vya umwagiliaji matone( drip irrigation)
Kufungiwa tank la Maji kuanzia lita 500,1000, 2000 n.k kutokana na ukubwa wa Greenhouse/Net house
Kupewa mbegu ya zao unalohitaji na yenye kutoa mazao mengi
Kufungiwa crop support
Kupandiwa
-Unakabidhiwa greenhouse/Net House ,ikiwa imekamilika
Kutembelewa na Kupewa ushauri wa mara kwa mara
Kupima Udongo
Kusaidiwa kutafuta Soko la Ndani Na Nje ya Nchi. Mfano kwa sasa tuna soko linalohitaji zaidi ya tani 3 za nyanya kila wiki. Nyanya zinazohitajika ni zile zinazopandwa kwenye greenhouse. Bado hakuna wakulima walioweza kuhudumia soko hilo
Tutakufuata popote pale ulipo Tanzania
Simu: 0763 071007
email: ushauri@kilimo.net

Response to "Faida za Greenhouse"

  • ahsante mtaalamu wetu wa kilimo ,sisi ni kikundi cha wanawake tunayo nethouse yenye ukubwa wa mita8kwa 15
    tunahitaji kupata ratiba ya kupanda mboga mboga kulingana na msimu,pia jinsi ya kupata mbegu chotara,jinsi ya kupima udongo tuko Shinyanga mjini , MAWASILIANO YETU NI 0787238867TUTAFURAHI KUPATA USHAURI AU UKIFIKA KUTUTEMBELEA

  • Mimi niko Morogoro, naomba kufahamu zilipo ofisi zenu ili niweze kufika kupata ushauri wa kilimo kwa kutumia greenhouse

  • Hizi ni zile za chuma mkuu?… Na gharama zinaeza rudi kwa muda gani?…

    Na shukuru kwa miembe inaendelea vizur kaka…

  • Leave a Reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *