Epuka hasara kwenye Kilimo Kwa Kufahamu jambo Hili Muhimu
Habari za leo mjasiriamali wa Kilimo. Ni matumaini yangu kabisa unaendelea vyema.
Leo napenda tujifunze jambo muhimu katika mafanikio ya kilimo. Nimekutana na wakulima wengi sana wakilalamika kuhusu kupata hasara kwenye kilimo chao au wamepata matokeo madogo sana kulinganisha na matarajio yao. Katika kutafuta sababu ni nini, nikagundua mambo kadhaa, ila moja wapo ni kwamba waliingia kwenye kilimo sababu waliona msimu huo kilimo hicho kimewapa watu hela nzuri, hivyo na wao wakaingia kwa matarajio ya kupata matokeo yaleyale au Zaidi. Ila badala yake mambo yakawa sivyo kabisa. Jambo ninalolizungumzia hapa ni kuhsu kujitofautisha, au kutofuata mkumbo wa wengine. Unapoingia kwenye kilimo siku zote usifuate mkumbo, Usione kila mtu kwa vile analima mahindi na wewe ukataka kulima mahindi, labda iwe ni kwa ajili ya chakula.
Lazima ujitofautishe na wengine, fanya kwa utofauti ikiwezekana nenda kinyume kabisa na wengine
Mfano Wakulima wengi wanapoona msimu huu zao la nyanya limekua na bei nzuri sana sokoni na kuna wakulima wamepiga hela nzuri, basi msimu huo wanaingia shambani kwa wingi wakiwa na matarajio yakupiga hela kama wale wenzao, bila kujua ni sababu zipi zimewafanya wakapiga hela nzuri. Kwa bahati mbaya wakishaingia kulima wote kwa mkumbo wanakivuna wanajikuta wote sokoni kila mtu ana nyanya, bei inaporomoka na wengi hula hasara.
Baada ya kula hasara wanaachana na kilimo cha nyanya, maana msimu ulikua mbovu kwao, na wanachukia kabisa kilimo cha nyanya. Msimu mwingine wale wakulima wengi walipata hasara hawalimi nyanya, wanabaki wale wajanja ambao pamoja nakupata hasara wana lima tena, msimu huu wanakutana na uhaba wa nyanya sokoni, maana wenzao walisusa sababu walikula hasara msimu uliopita. Sababu ya uhaba wa nyanya sokoni bei ya nyanya inakua juu wanapata kipato kizuri. Mzunguko unaendelea.
Hapa kuna jambo kubwa sana la kujifunza, ambalo ni kujitofautisha na wengine au kwenda kinyume kabisa na wakulima wengine. Mfano ukiona msimu huu kila mtu anaongelea kulima zao fulani kwa sababu limekua na pesa nyingi sana, basi wewe achana na kilimo hicho tafuta zao lingine ambalo unajua watu hawalizungumzii au kwa msimu huo limewapa watu hasara. Mfano ikitokea msimu huu vitunguu watu wamepata hasara na wanalalamika soko halikua zuri sababu vitunguu vilikua vingi sokoni basi wewe ndio wakati wa kwenda kulima zao hilo. Kwa kawaida Vitunguu hua na bei nzuri miezi ya December, January, February, March, April na May. Sasa Ikitokea mwaka huu kwenye miezi hiyo labda bei zikaporomoka sana sababu ya kuwa na vitunguu vingi sana sokoni basi msimu ujao wewe kalime vitunguu. Ila ikitokea kwamba mwaka huu vitunguuu vimekua na bei kubwa sana, basi msimu unaofuata usiende kulima vitunguu. Labda kama una soko lako maalumu ambalo unauza kwa makubaliano maalumu au mkataba.
Inapotokea msimu huu umelima vitunguu na umepata hasara sababu bei ziliporomoka, basi usikate tamaa, lima tena.
Kumbuka nazungumzia kujitofautisha, na kujitofautisha kupo kwa aina nyingi na katika hatua nyingi za kilimo, kuanzia kwenye kulima hadi sokoni. Lakini kwa leo tumeongelea kujitofautisha kwenye kipengele cha mismu ya kulima. Wakati mwingine tutaangazia namna ya Kujitofautisha kwenye hatua nyingine za kilimo na sokoni.
MUHIMU: Leo ndio Mwisho wa OFA ya Vitabu vipya
Vitabu hivyo ni:
1. Mwongozo wa Kilimo cha Tikiti Maji
2. Mwongozo wa Kilimo Biashara cha Vitunguu Maji
Toka vilivyozinduliwa vimekua vikipatikana kwa bei ya OFA ya 10,000 tu kwa kitabu kimoja badala ya 15,000 kwa kila kimoja. OFA hiyo inaisha Leo tarehe 15 September 2017. Jitahidi leo upate nakala yako.
Namna ya Kupata nakala yako:
Vitabu hivi vinapatikana kwa njia ya Mtandao (email, WhatsApp au telegram). Yaani unatumiwa kwenye email yako au WhatsApp yako au telegram. Ndani ya dakika 5 baada ya kulipia unakua umepata nakala yako popote ulipo duniani.
Unafanya malipo ya 20,000 Kwa vitabu viwili (au 10,000 kwa Kitabu Kimoja) kupitia mpesa 0763 071007 au Tigo pesa 0712578307 (Jina Litaonyesha Daudi Mwakalinga)
Ukishafanya malipo unatuma Ujumbe wenye Jina na email yako kwenda 0763 071007 au 0712 578307. Kama huna email na ungependa kutumiwa Kitabu kwa Whatsapp au Telegram basi unatuma ujumbe WhatsApp au Telgram kwenda namba 0763 071007. Karibu sana.
Kwa ushauri kuhusu kilimo wasiliana nasi kupitia:
Simu 0763 071 007
email: ushauri@kilimo.net
Karibu sana:
Response to "Epuka hasara kwenye Kilimo Kwa Kufahamu jambo Hili Muhimu"
Maoni mazuri sn, hasa katika masoko ambayo kwa kiasi fulani hubadilika badilika, nimeupenda japo binafsi napenda sana kulima kitunguu swaumu ambacho nadhani kina soko zuri zaidi ya kitunguu maji, hasa maeneo ya nchi jirani, hivi hizi mbegu mnazo hapo? Na je, vp kwa ukanda huu wa nyanda za juu kusini hasa Mbozi ambako kuna udongo wa mfinyanzi vinastawi ktk ardhi hii? Na kama mbegu inapatikana ni kiasi gani?