Kilimo Bora cha Nyanya, Lima Kitaalamu na Kibiashara
Utangulizi:
Nyanya ni zao la mboga ambalo hulimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Inahisiwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.
Uzalishaji wa nyanya duniani na hapa Tanzania
Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa nchi zinazo lima ni kama; Malawi, Zambia na Botswana.
Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.
Zao la nyanya linalimwa karibu maeneo yote ya Tanzania. Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni jumla ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya kilimo ya Tanzania maeneo yanalolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida. Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 (ekari 15,398). Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana.
Uzalishaji mdogo unasababishwa na kupungua kwa rutuba ya ardhi, upepo, joto, ukame. Sababu nyingine ni pamoja na ukosefu wa aina za nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu, wadudu, magonjwa na magugu.
Hali ya Hewa:
Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.)
Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 – 7.0.
Kotokana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika makundi mawaili:
1. OPV (Open Pollinated Variety) – Aina za kawaida. Mfano Tanya, Mwanga, Onyx n.k
2. Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno, mengi, zilizoboreshwa zaidi. kati ya hizo zipo aina fupi,za kati na ndefu. Mfano Victory F1, Anna F1, Kipato F1, Monica F1, Kilele F1 n.k
1. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF n.k. Hizi huweza kuvunwa mara 2 hadi 3.
Mambo muhimu ya kuzingatia:
• Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu
• Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha
• Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo.
• Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.)
• Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia
kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine.
Aina ya matuta:
– matuta ya makingo (sunken seed bed)
– matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed)
– matuta ya kawaida (flat seed beds)
Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta
• Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyaga miche].
• Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini.
• Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu.
• Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo.
• Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba.
• Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota.
– matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi.
– Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi
– Matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara.
– Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo kama hayakutengenezwa vizuri.
Faida:
· matuta haya ni rahisi kutengeneza
· hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu
· nyevu mdogo unaopatikana ardhini
· ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba
· huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu
· huzuia mmomonyoka wa ardhi
Hasara:
· Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi.
3. Matuta ya kawaida (flat seed beds):
Faida:
· ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa
· na kusambazwa mbegu huoteshwa
· ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu
Hasara:
Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi.
• Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni (germination test)
• Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari
• Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2
• Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can).
• Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta.
Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza msongamano. Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi kama vile kinyausi (damping off) au ukungu (blight).
• Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa
mbegu.
• Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini
• Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye udongo.
• Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga. (kipindi cha baridi si muhimu sana)
• Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 – 4. Hii itapunguza magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na yenye nguvu.
• Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia shambani.
• Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10.
• Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche.
• Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya.
• Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya.
• Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. Kama ni kipindi cha baridi ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzungungo wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi.
Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani (TransplantingRules)
• Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri na udongo.
• Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa katika nafasi zinazo stahili huko shambani.
• Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na jua.
• Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na mizizi mingi iliyostawi vizuri.
• Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa kupeleka shambani.
• Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
• Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa toka kitaluni.
• Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili kutoharibu miche/mizizi.
• Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
• Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
• Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa bustanini.
• Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua.
• Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema
• Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini.
• Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto.
• Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu.
ni yakioza yanakua mbolea nzuri na kurutubisha ardhi. Uwekaji wa matandazo una ufanisi kwenye kilimo cha eneo dogo, ila kwa maeneo makubwa, upatikanaji wa matandazo unakawa ni changamoto.
Uwekaji wa miti unasaidia ukuaji wa nyanya na hivyo kupelekea kuzaa zaidi. Kwa aina ndefu za nyanya uwekaji miti hauepukiki ni lazima uweke miti ya kueleweka ambayo itaruhusu ukuaji mzuri, pia miti lazima iwe imara ili kuweza kustahimili mzigo wa nyanya pindi nyanya itakapokua imezaa vizuri. Kwa nyanya fupi (determinate) na saizi ya kati (semi determinate kwa mfano kipato F1) Tumia fito ndefu (mt 1.5) na nene (cm 4-5) pamoja na kamba ngumu hasa za katani au kudu.
Kwa nyanya ndefu ( indeterminate mfano victory F1, Anna F1) ni bora zaidi utumie nguzo nene/milunda urefu Mt 2.5 unene sm 10-12 pamoja na waya na kamba nzuri za kudu ( zitatengeneza umbo kama la njia ya umeme). zoezi lifanyike kabla ya mimea kuanza kuweka maua
Upotevu wa mazao baada ya kuvunwa husababishwa hasa na utunzaji duni wa mazao hayo, njia duni za usafirishaji, pamoja na kuchelewa kuvuna. Kupunguza upotevu unashauriwa kuvuna kwa wakati nyanya zako. Maana nyanya zilizoiva sana, ni rahisi kuharibika wakati wa uvunaji na hata wakati wa kusafirisha maana ganda lake la nje linakua ni laini. Kama soko lako liko mbali vuna nyanya zikiwa ndio zimeanza kuonyesha dalili ya kuiva maana wakati huo nyanya inakua na ganda gumu hivyo kuweza kuvumilia mikikimikiki ya usafirishaji. Lakini pia nyanya itaweza kukaa muda mrefu zaidi bila kuharibika ikilinganishwa na ile iliyovunwa ikiwa imeiva sana. Ila pia zipo aina za nyanya zinazokaa muda mrefu wa hadi wiki 3 bila kuharibika kama zikitunzwa vizuri.
Pichani ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Peter Msigwa ambaye ni mkulima mzuri wa nyanya |
- Je Ungependa kulima Kilimo cha Uhakika Cha Zao lolote? Hata kama huna elimu ya Kilimo?
- Je ungependa kufahamu mtaji unaohitajika kwenye kilimo cha Nyanya au mazao emngine na namna unavyoweza kujua makadirio ya faida utakayoipata?
- Je unatamani Kulima kilimo biashara cha zao lolote ila hujui uanzie wapi?
- Watu wengi hua wanasikia stori za namna ya kupata faida kubwa kwenye kilimo, lakini wakiingia wanajikuta hawapati matokeo sawa na walivyosikia zile stori/hadhithi. Na wakati mwingine wanapata hasara kabisa. Je unajua kwanini?
Huduma ya Kwanza: Uchambuzi wa Gharama na Faida (Cost benefit Analysis – CBA) wa Zao lla Nyanya.
Kwanini CBA? Baadhi ya Manufaa ya kuanza na CBA ni:
- CBA itakusaidia kujua Rasilimali na gharama zinazohitajika kwenye uwekezaji wa kilimo unachotaka kufanya. Hii itakusaidia kufanya maamuzi ya kuendelea na wazo la kulima zao hilo au itakubidi ufanye zao lingine.
- CBA itakusaidia kujua makadirio ya mapato faida utakayopata. Hakuna mtu anayependa kufanya kitu bila kujua manufaa ya kile anachokifanya. Hivyo CBA itakupa picha ya kile utakachokipata.
- CBA itakusaidia kujua mgawanyiko wa gharama zinazohitajika. Mfano kama kilimo cha Nyanya kinahitaji mtaji wa milioni 2. Haina maana kwamba lazima uwe na hizo milioni mbili ndio uanze kilimo cha Nyanya. Inaweza kua inahitajika laki 5, halafu baada ya mwezi ikahitajika milioni moja, halafu mwishowe ikahitajika laki 5. Sasa bila kujua mgawanyiko huo unaweza kudhani ni ngumu kufanya kilimo cha Nyanya kwasababu ya mtaji mkubwa unaohitajika, kumbe unaweza kuanza na kiasi fulani. CBA itakupa picha kamili kwenye hilo.
Huduma hii pia inaambatana na ushauri wa mbegu nzuri kulingana na soko unalolilenga na ukuaji wake kwenye eneo unalotaka kulima. Pia namna ya kuipata mbegu Halisi (maana moja ya changamoto kwenye kilimo ni kwamba baadhi ya mbegu ni feki, unaweza kununua mbegu ghali na mwishowe kumbe umechukua feki)
Huduma ya Pili: Master Plan. Huu ni Muongozo au Mpango kazi wa Kilimo cha zao la Nyanya.
Mpango au Muongozo huu unakuonyesha shughuli zote za Shambani na muda wake wa kufanyika. Hii itawasaidia sana wale ambao wanataka kufanya kilimo lakini hawajui kipi kianze na kipi kifuate. Pia utawasaidia kuongeza faida wale ambao wamewahi kulima kilimo cha nyanya lakini hawakupata faida waliyotegemea. Muongozo huu utakuonyesha aina ya mbolea na kiasi kinachohitajika, aina za madawa ya magonjwa na wadudu na kiasi gani cha uchang
anyaji wa dawa hizo, Umwagiliaji, na mambo mengine mengi.
Huduma hii ya Master Plan, pia inaambatana na ushauri wa aina zote za mbolea sahihi zinazohitajika na kiasi cha uwekaji kwa kila mmea, Pia madawa yote yakayohitajika kuanzia wakati wa kupanda hadi wakati wa kuvuna. Shughuli hizi na nyingine zimewekwa kwa mtiririko mzuri kwendana na wakati shughuli hiyo inapohitajika
Kwa Huduma zote mbili Gharama yake ni 30,000/= (Elfu thelathini tu)
Pia CBA na Master Plan za Kitunguu, Pilipili Hoho na Tikiti Maji zipo tayari.
Huduma hizi zinaweza kumfikia mkulima popote pale alipo kwa kutumia njia ya email. Wenye simu zenye kusoma mafaili ya mfumo wa pdf, tunawatumai kupitia whatsapp au Facebook. Malipo yanafanyika kwa njia ya MPESA kupitia namba 0763 071 007. Huduma hizi zinamfikia mteja ndani ya dakika 15 baada ya kufanya malipo.
BONUS: Kwa wale watakaochukua Huduma hizi kuanzia tarehe 18 hadi 31 December 2016, watapa Bonus ya Jarida la Kilimo cha Bustani Bure. Jarida au Kijitabu hichi ni cha kiswahili na kimeandikwa vizuri sana. Topic zilizopo kwenye Jarida hilo ni hizi zifuatazo:
- KITALU CHA MBOGA NA MATUNDA (Maandalizi ya kitalu na matunzo ya miche.)
- KILIMO BORA CHA NYANYA
- KILIMO BORA CHA VITUNGUU .
- UZALISHAJI WA MBOGA ZA MAJANI
- UZALISHAJI WA UYOGA.
- MBINU ZA MSINGI ZA KUTHIBITI MAGONJWA NA WADUDU KATIKA KILIMO CHA MBOGA
- MBINU ZA KUVUNA NA KUHIFADHI MBOGA .
- MASOKO YA MBOGA NA MATUNDA
Kwa swali lolote kuhusu kilimo au ushauri, au kupata huduma zetu Waweza kuwasiliana nasi kwa Namba 0763 071007 au kupitia email yetu: ushauri@kilimo.net
Asante na Karibu sana.
www.kilimo.net
Response to "Kilimo Bora cha Nyanya, Lima Kitaalamu na Kibiashara"
PONGEZI SANA KWA KILIMO
Nashukuru
Mkuu hongera sana kwa kazi hii,
Hakika tunapata jifunza mengi hapa.
Mungu aibariki hii kazi yako ,
Tushindwe sisi tu .
nmejisikia vizuri sana mkuu