OFA! OFA! OFA! Ni OFA ya PASAKA kwa kila mkulima

OFA! OFA! OFA! Ni OFA ya PASAKA kwa kila mkulima

Habari za leo mdau wa kilimonatumaini unaendelea vyema.
Leo ni siku nyingine ambayo Mwenyezi Mungu ametubariki nayo. Kabla sijakuletea OFA ya Pasaka, napenda kukushirikisha moja ya misingi ya muhimu katika mafanikio ya jambo lolote. Je unajua kwanini wanaofanikiwa ni wachache kuliko wasiofanikiwa? Ni kwasababu waliofanikiwa wana siri/tabia za tofauti na wasiofanikiwa. Moja ya tabia/siri ya wanaofanikiwa ni kujifunza bila kukoma (continuous learning), ni watu wa kusaka maarifa kila wakati. Mfano unataka kuwekeza kwenye kilimo, je una maarifa ya kutosha kuhusu kilimo unachotaka kufanya? Au umesikia tu kilimo cha zao fulani kinalipa sana, ukahamasika ukataka na wewe utumbukie huko? Wengi hufanya hivyo, baada ya kuhamasika kwamba kilimo fulani kinalipa, hukimbilia kuwekeza pesa zao huko bila kusaka kwanza maarifa ya kutosha, na mwishowe wengi huambulia hasara. Nimekutana na watu wengi sana ambao waliingia kwenye kilimo sababu walihamasika kwamba kilimo fulani kinalipa, na mwisho wake walikula hasara kubwa. Katika hao wote niligundua baadhi ya visababishi vya msingi (main causes) vilivyowapelekea kupata hasara, na kisababishi kikubwa kuliko vyote ni kukosa maarifaa/ elimu ya kutosha kuhusu kilimo walichofanya. Baadhi yao nilianza kuwaelemisha hatua kwa hatua (coaching), na wakaanza tena kilimo, wengine nilifika shambani mara kadhaa na hatimaye matokeo yalikua ni mazuri sana. Katika kufikiri namna ninavyoweza kutatua changamoto hii kwa watu wengi zaidi, ndipo nikapata wazo la kuandika vitabu hivi. Kitaaluma mimi ni mtaalamu wa kilimo, nina shahada ya kilimo cha mazao ya bustani (Bsc. Horticulture) kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine Morogoro, lakini pia nina uzoefu wa kufanya kazi na wakulima wadogo, wa kati, na wakubwa kwa zaidi ya miaka 6 sasa. Kiukweli hakuna kitu kinanikosha moyo (kinanifurahisha), kama kupata mrejesho mzuri wa watu walivyofaidika na ushauri na utaalamu ninaoutoa kwa watu mbalimbali.
Ngoja nisikuchoshe na mastori mengi, ila kwa kifupi tu vitabu hivi ukisoma na kufuatilia ushauri uliopo ndani yake, kupata faida kwenye kilimo chako ni jambo la uhakika kwa asilimia100%. Mirejesho mizuri ninayoipata kutoka kwa wakulima waliotumia mbinu zilizopo kwenye vitabu hivi ndio inayonipa hamasa zaidi ya kuwafikia watu wengi zaidi.
Vitabu vilivyopo kwenye OFA ya Pasaka ni vitabu 3:
1. Mwongozo wa kilimo biashara cha Vitunguu maji
2. Mwongozo wa Kilimo cha TIkiti maji
3. Mwongozo wa Kilimo cha Nyanya
Vitabu vyote hivi 3 unavitapata kwa 20,000 tu badala ya 45,000.
Namna ya Kupata nakala zako:
Vitabu hivi vinapatikana kwa njia ya mtandao (email, telegram, au Whatsapp) Yaani unatumiwa kwenye email au whatsapp.
Unafanya malipo ya 20,000 Kwa mpesa 0763 071007 au Tigo pesa 0712578307 (Jina Litaonyesha Daudi Mwakalinga)
Ukishafanya malipo unatuma Ujumbe wenye Jina na email yako kwenda 0763 071007 au 0712 578307.
Kama huna email na ungependa kutumiwa Kitabu kwa Whatsapp basi utatuma ujumbe WhatsApp kwenda namba 0763 071007. VItabu utavipata ndani ya dakika 5 hadi 10 baada ya kufanya malipo.
Wahi Ujipatie nakala zako kwa bei ya OFA. Mwisho wa OFa ni 8.04.2018
Ikiwa utapenda kuchukua kitabu kimoja, basi utapatiwa ofa ya 10,000 badala ya 15,000. Ikiwa utahitaji vitabu 2 tu, utapata ofa ya 15,000 badala ya 30,000.
Ni mimi Mtaalamu wako Daudi Mwakalinga (0763 071007). Tukutane wakati mwingine.Karibu sana
 
Hapa chini nimekuwekea ufafanuzi kidogo wa baadhi ya mambo yaliyomo kwa kila kitabu

Mwongozo wa Kilimo cha Nyanya

Baadhi ya Mambo utakayojifunza kwenye Kitabu hiki:

  • Utajifunza kuhsu sifa za udongo, Mazingira, hali ya hewa, inayofaa kwa ajili ya kilimo cha Nyanya.
  • Aina za nyanya, na nyanya zinazofaa kwa biashara.
  • Utajifunza namna ya kuandaa kitalu kizuri cha nyanya.
  • Utafahamu aina 3 za matuta ya vitalu vya miche ya nyanya, vilevile utafahamu namna ya kutunza miche kitaluni.
  • Utajifunza Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani. Hii itasaidia kuepuka miche kufa baada ya kuhamishia shambani. Miche yako itastawi vizuri
  • Utazifahamu na kujifunza mbinu mbalimbali za utunzaji wa shamba lako ili kuongeza uzalishaji.
  • Utafahamu wadudu na magonjwa sumbufu kwenye nyanya, na namna ya kuyathibiti.
  • Uvunaji, na utunzaji wa nyanya baada ya kuvuna. Utajifunza namna ya kuepuka upotevu wa nyanya baada ya kuvuna
  • Masoko: Hapo utafahamu masoko mbalimbali ambapo nyanya zinauzika.
  • Mienendo ya Bei; Utajifunza namna bei za nyanya zinavyobadilikabadilika kwa mwaka mzima. Kipindi gani cha Bei nzuri na kipindi cha bei ndogo
  • Utajifunza namna ya kupata taarifa za soko na wanunuzi kwa kutumia simu yako ya simu: Hapa utaweza kupata mawasiliano ya wanunuzi wa nyanya kupitia simu yako. Pia bei za kila siku za nyanya kutoka kwenye masoko makubwa hapa nchini.
  • Utafahamu ni msimu gani mzuri wa kupanda nyanya ili kukutana na bei nzuri sokoni na wewe unufaike kwa faida kubwa.
  • Utafhamu mchanganuo wa gharama na faida kwenye kilimo cha nyanya ekari moja. Hii itakupa picha, kujua kiasi cha mtaji unachopaswa kuwa nacho ili kulima nayanya, Pia utafahamu faida utakayopata

Mwongozo wa Kilimo cha TIkti Maji

Baadhi ya Yaliyomo kwenye Kitabu hiki:

  • Utajifunza shughuli zote za shambani kuanzia kuandaa shamba, upandaji, umwagiliaji, uwekaji mbolea, palizi, uvunaji n.k
  • Vigezo vya kuzingatia katika uchaguaji wa shamba zuri pamoja na mbegu nzuri
  • Utawafahamu Wadudu waharibufu na namna ya kuwadhibiti kikamilifu, pia Magonjwa yanayoathiri sana tikiti maji na namna ya kuyathibiti
  • Utajifunza uchavushaji (pollination) kwenye zao la tikiti maji na namna unavyoweza kuongeza uchavushaji na kuongeza mavuno hadi asilimia themanini (80%)
  • Masoko: Utaelewa mienendo ya bei, kipindi chenye bei nzuri, kipindi chenye bei mbaya na sababu zake. Hii itakusaidia kujua wakati sahihi wa kupanda zao la tikiti ili upate faida nzuri Zaidi.
  • Utajifunza namna unavyoweza kutumia simu yako kujua bei za tikiti kwenye masoko yote hapa Tanzania. Yaani bei za kila siku za kwenye masoko yote makubwa hapa Tanzania utaweza kuzijua kupitia simu yako.
  • Pia utajifunza namna ya kutafuta wanunuzi kupitia simu yako, yaani utajua namna ya kupata mawasiliano ya wanunuzi(namba zao za simu) kutoka masoko mbalimbali. Kwenye kitabu hichi utajifunza hayo yote.
  • Master plan: Hapa mwandishi amekuwekea mpangilio wa shughuli zote, tena hatua kwa hatua kuanzia kupanda hadi kuvuna. Utafahamu nini kianze na kipi kifuate. madawa yote, mbolea zote, na shhguli nyingine zote zipo
  • Uchambuzi wa gharama na Faida: Hapa utapata kufahamu rasilimali zote zinazohitajika na gharama zake, pia utajua kiasi cha faida utakayopata.

 

Mwongo wa Kilimo Biashara cha Vitunguu maji

Baadhi ya Yaliyomo kwenye Kitabu hiki:

  • Utajifunza namna ya kuandaa kitalu bora cha miche ya vitunguu na jinsi ya kutunza kitalu hadi kuhamisha miche kwenda shambani
  • Utajifunza shughuli zote za shambani kkama kuandaa kitalu, shamba, upandaji, umwagiliaji, uwekaji mbolea, palizi, uvunaji n.k
  • Vigezo vya kuzingatia katika uchaguaji wa shamba zuri pamoja na mbegu nzuri
  • Utazijua aina za mbegu mbalimbali na utazijua mbegu nzuri zinazofanya vizuri maeneo mengi na kampuni zinazotengeza mbegu hizo
  • Utawafahamu Wadudu waharibufu na namna ya kuwadhibiti kikamilifu, pia Magonjwa yanayoathiri sana Vitunguu maji na namna ya kuyathibiti
  • Masoko: Utaelewa mienendo ya bei, kipindi chenye bei nzuri, kipindi chenye bei mbaya na sababu zake. Hii itakusaidia kujua wakati sahihi wa kupanda zao la vitunguu ili upate faida nzuri Zaidi.
  • Utajifunza namna unavyoweza kutumia simu yako kujua bei za Vitunguu kwenye masoko yote hapa Tanzania. Yaani bei za siku hiyo kwenye masoko yote makubwa hapa Tanzania utaweza kuzijua kupitia simu yako.
  • Wanunuzi: utajifunza namna ya kutafuta wanunuzi wa vitunguu kupitia simu yako,
  • Master plan: Hapa mwandishi amekuwekea mpangilio wa shughuli zote, tena hatua kwa hatua kuanzia kupanda hadi kuvuna. Utafahamu nini kianze na kipi kifuate.
  • Uchambuzi wa gharama na Faida: Hapa utapata kufahamu rasilimali zote zinazohitajika kwa zao la kitunguu na gharama zake, pia utajua faida utakayopata.

No comments.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *