KILIMO UHAKIKA – Karibu tufanye kazi

KILIMO UHAKIKA – Karibu tufanye kazi

Kilimo Uhakika (KiU) ni mpango wa mafunzo na ushauri wa kilimo, ambapo mshauri wako wa kilimo Kocha Daudi Mwakalinga akishirikiana na wataalamu wengine wa kilimo.net Wanakupa mafunzo na mwongozo wa kuweza kufanya kilimo cha uhakika. Mafunzo haya ni kwa mwaka mzima.
Baadhi ya YALIYOMO kwenye program ya KILIMO UHAKIKA

  1. Online Library (Maktaba ya Mtandaoni) – Hii ni maktaba ya vitabu, audio, picha na Video za mafunzo ya kilimo biashara na ufugaji. Kila mwanachama wa Kilimo Uhakika (KiU) ataweza kuingia kwenye mkataba hiyo kupitia simu au computer yake. Kila Mwezi kutakua na masomo mapya yatakayowekwa kwenye Maktaba hii.

Huo ni mwenekano wa sasa wa Masomo yaliyopo mpaka sasa. Tuendelea kuongeza masomo


 

Hapo Juu ni Muonekano wa baadhi ya masomo kuhusu Vitunguu maji


2. Makala Maalumu za Kilimo: Wanachama wa KiU watakua na Ukurasa wao maalumu ambao utakua unawekwa Makala za kilimo ambazo Mwanachama wa KiU peke yake ndio ataweza kuziona. Kila mjumbe atakua na password yake kwa ajili ya kumuwezesha kusoma Makala hizo. Makala hizi zitakua tofauti na zile zinazowekwa kwenye blog ya kilimo.net kwa ajili ya wasomaji wa kawaida.
3. Vitabu 2 Kila mwezi. Vitabu hivi ni vya nakala tete (soft copy) ambapo vitakua vinatumwa kwenye email za wanachama, pia vinawekwa kwenye Online Library ya Kilimo Uhakika
4. OFA za Matangazo ya Bidhaa na Huduma. Mwanachama wa Kilimo Uhakika, atapata OFA ya kutangaziwa bure bidhaa au huduma zake kwenye mitandao ya kilimo.net (Facebook, Blog na Email). 1. Kupitia ukurasa wetu wa FB tunaweza kuwafikia watu Zaidi ya 300,000 kwa wiki, 2. Kupitia Blog (kilimo.net) ambayo kila siku tunaweza kufikia watu 600 hadi 800, na 3.Kupitia mfumo wetu wa email ambapo tunaweza kuwafikia watu Zaidi ya 7,000 kupitia email. Bidhaa au huduma zitakazotangazwa ni zile zinazohusiana na kilimo au ufugaji. Sasa hivi Kwa ambaye si mwanachama tangazo moja ni 50,000 hadi 100,000 kwa wiki moja. Ila kwa Mwanachama wa Kilimo Uhakika atatangaziwa matangazo yasiyozidi 3 bure kwa mwaka.
5. Kundi la Whatsapp: Kila mwanachama atapata fursa ya kuwepo kwenye Kundi la Whatsapp la KILIMO UHAKIKA, ambapo mafunzo mbalimbali yatakua yanatolewa kwenye kundi la Whatsapp.
6. Watapata OFA ya kulipa Nusu Bei kwenye Semina zitakazokua zikiendeshwa na Kilimobiashara.net: Kwa mwaka kutakua na semina 4 za kilimo biashara. Mfano kama semina moja inagharimu 40,000, basi mwanachama wa Kilimo Uhakika atalipia nusu yaani 20,000 tu
7. Ofa ya Vitabu 2 vitakavyotolewa mwaka huu. Tunategemea Mwaka huu kabla haujaisha tuwe na vitabu angalau 4 vya masomo mbalimbali. Vitabu hivi kila mjumbe wa KiU atapata vitabu 2 bure kabisa.
8. Kila Mwezi, tutakua na Mafunzo ya Kilimo ambapo tutakua na mtaalamu aliyebobea kwenye mada husika.
9. Kila Mwezi tutashirikishana uzoefu wa wakulima waliofanikiwa vizuri katika kilimo cha zao Fulani au ufugaji. Hapa Kila mwezi tutakua na mkulima au mfugaji aliyepata mafanikio makubwa katika kilimo cha zao fulani au ufugaji
10. Kila mwanachama atatengenezewa email yake ambayo itakua kwa ajili ya kupata maarifa na taarifa za Kilimo Uhakika. Email hizi zitaishia na domain ya kilimo.net (Mfano: daudi@kilimo.net)
11. Fursa mbalimbali za Kilimo. Wanachama wa Kilimo Uhakika (KiU) watapata kipaumbele katika kupewa fursa zozote za kilimo biashara zilizopo na zitakazoendelea kujitokeza. Mfano fursa za masoko mbalimbali ya mazao na mifugo
12. Swali lolote kuhusu kilimo lazima lipatiwe ufumbuzi. Kwa changamoto yoyote ya kilimo au Ufugaji ambayo mwanachama ataipata atapata ushauri.
13. Kila mwanachama atapata nafasi ya kushiriki katika kuandaa na kutekeleza mradi wa pamoja. Hapa Wanachama tutabuni mradi wa kilimo ambao tutaufanya kwa kushirikiana.
14. Tutafanya tathimini ya kila mwanachama kujua wapi amefanikisha na wapi amekwama na nini kifanyike. Tutakua na Tathimini ya kila baada ya miezi 3.
Sifa za kuwa mwanachama wa Kilimo Uhakika
Lazima uwe na kiu ya kufanikiwa. Uwe na dhamira ya kweli ya kutoka hapo ulipo na kwenda hatua ya juu zaidi
Lazima uwe mtu wa kupenda kutafuta maarifa (Kujifunza)
Lazima uwe mtu wa kuchukua hatua. Lengo la kujifunza ni kufanyia kazi mafunzo haya. Mabadiliko ni lazima yaonekane
Namna ya Kujiunga na Kilimo Uhakika
Ili kuwa mwanachama wa Kilimo Uhakika, utalipia Ada ya 50,000, hii ni Ada ya Mwaka mzima (yaani miezi 12 tangu tarehe uliyojiunga). Malipo yanafanyika kwa MPESA kwenda namba 0763 071007 (Jina litaonyesha Daudi Mwakalinga). Ukishafanya Malipo Utatuma meseji ya Muamala itakayorudi kwako baada ya kulipia. Unapofanya malipo kuna ile meseji ya uthibitisho kwamba malipo yamefanyika, tutaomba meseji hiyo uitume kwenda 0763 071007.
Baada ya hapo utatuma pia SMS yenye Jina na email yako kwenye namba 0763 071007, na uanachama wako utaidhinishwa rasmi.
Karibu sana kwenye KILIMO UHAKIKA tufanye kazi pamoja.
Kauli mbiu yetu: Mafanikio ni Haki Yetu

Response to "KILIMO UHAKIKA – Karibu tufanye kazi"

    • Habari Ndugu Mariki David, Unaweza kulipia kwa njia ya bank. Ikiwa bado wahitaji kujiunga nijulishe tukupatie details za bnak kwa ajili ya kulipia. Asante sana

  • Leave a Reply to kilimobiashara Cancel reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *