FURSA KUPITIA TEKNOLOJIA YA KILIMO CHA GREENHOUSE

FURSA KUPITIA TEKNOLOJIA YA KILIMO CHA GREENHOUSE

Habari ndugu mjasiriamali wa kilimo ni matumaini yangu unaendelea vizuri na mapambano ya kuelekea kwenye mafanikio kupitia kilimo. Karibu tena katika kona hii ya kupata maarifa ya kilimo. Kutokana na maombi na maswali kadhaa ya watu kuhusu Kilimo cha Greenhouse, leo nitapenda tuanze kujifunza kuhusu mada hiyo ya Greenhouse. Leo tutaangazia kwanza maana ya teknolojia hiyo, historia yake, faida zake, Aina zake, pamoja na matumizi na mapato kwa baadhi ya Greenhouse
Karibu sana:
Kwanza tuanze kwa kupata tafsiri ya neno lenyewe, Greenhouse imekua ikipatiwa majina tofauti tofauti, wapo watu wanaiitaNyumba ya Kijani, wengine wanaiitaBanda Kitalun.k Vyovyote utakavyopenda kuiita teknolojia hii, cha muhimu ni kuelewa nini hasa maana yake.
Greenhouse(Banda Kitalu):ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa. Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.
Teknolojia hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi baridi, zaidi ya karne moja na nusu (miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi, mazao ya kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani kabisa kulimwa maeneo hayo ya ukanda wa baridi. Ndipo hapo wazo la kuvumbua Greenhouse lilipoibuka. Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kijani ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi. Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna utofauti kati yake na zile za nchi za ukanda wa baridi.
Faida au fursa za Greenhouse

  1. Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi, ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.
  2. Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya uharibifu wa mazao.
  3. Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
  4. Uwezo wa kupata soko zuri la mazao. Greenhouse itakuwezesha kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu,ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei nzuri
  5. Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti.
  6. Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti wake ni rahisi. Miundombinu ya umwagiliaji inayotumika hapa ni umwagiliaji wa matone (drip irrigation) ambapo maji yanakwenda pale penye mmea tu.
  7. Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili ya kuzoea mazingira ya nje kwanza.
  8. Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (soilless culture).Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuziwa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea.
Baadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo chaGreenhouse.

  • Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri kupitia teknolojia hii. Tuanze na Marekani, Marekani ina eneo takribani 4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua, Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni 2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka. Nchini Hispania inakadiriwa zaidi 25,000hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwagreenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe machanga,pamoja na nyanya.
  • Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapohazilimwi kwingine. Mazao maarufuyanayolimwa kwenye Greenhouse za Canada kama nyanya, matango na hoho.
  • Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse. Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi ndio nchi inayoongoza kwa teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana. Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga, pamoja na mbegu. Mfano : Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower, Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)
  • Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua (cut flowers) nje ya nchi. Japokuwanchi ya Israel eneo lake kubwa ni jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse. Balton Tanzania yenye makao yake makuu mjini Arusha, ni moja ya kampuni toka Israel zinazofanya vizuri katika sekta hii.
  • Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao ya yanya na tango yanalimwa kwenye green house.
  • Misri10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse.Nchi nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kamaJapan (40,000hekta) na Korea kusini (21,000 hekta).
Aina za Greenhouse.
Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo:

  1. Aina za Greenhouse kwakigezo cha sura/umbile (shape)

Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu

  • Quonset Greenhouse
  • Saw tooth type
  • Even span type greenhouse
  • Uneven span type greenhouse
  1. Aina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi
  • Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)
  • Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)
  1. Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)
  • Greenhouse za miti (Wooden framed structure)
  • Pipe framed structure (Greenhouse zinazotumia mabomba)
  • Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma)
  1. Aina za Greenhouse kwa kigezocha aina ya zana za ufunikaji (covering types)
  • Greenhouse zinazofunikwa kwazana za Vioo (Glass Greenhouse or Screenhouse) )- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza joto kwa muda mrefu ndanigreenhouse
  • Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya plaski (plastic film)
  1. Aina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa:
  • Greenhouse za gharama kubwa (High cost greenhouse) ( Zaidi ya milioni 50)
  • Greenhouse za gharama za kati (medium cost greenhouse) (milioni 20 hadi 50)
  • Greenhouse za gharama ndogo (Low cost greenhouse) (chini ya milioni 20)

Greenhouse za gharama ndogo ndio watu wengi wanazitumia sana katika nchi zinazoendelea.

Kwa wanaohitaji greenhouse Na Net house, bei zake ni kama ifuatavyo:
Greenhouse na Nethouse za bei nafuu.
Ukubwa wa Greenhouse na bei zake:
Mita 6 kwa 12 Milioni 4.2
Mita 6 kwa 24 – Milioni 6.2M
Mita 8 kwa 15 Milioni 5.5
Mita 8 kwa 30 Milioni 12.5
Mita 16 kwa 30 -Milioni 17
NET HOUSE Hizi zinafaa sana kwa yale maeneo ya joto.
Mita 6 kwa 12- Milioni 3.9
Mita 8 kwa 15 Milioni 5.0
Mita 8 kwa 30- Milioni 11
Mita 16 kwa 30 Milioni 15
NB: Tutakufungia Ukubwa wowote unaotaka kulingana na bajeti yako
Package inakuwa Na vitu vifuatavyo:
Utapewa Elimu Kwanza ya Kutosha Greenhouse/ Net House na Drip Irrigation
-Kujengewa greenhouse / Net house Kwa kutumia Miti Imara ya Miti, inayodumu Kwa Miaka kuanzia 15.
Kufungiwa vifaa vya umwagiliaji matone( drip irrigation)
Kufungiwa tank la Maji kuanzia lita 500,1000, 2000 n.k kutokana na ukubwa wa Greenhouse/Net house
Kupewa mbegu ya zao unalohitaji na yenye kutoa mazao mengi
Kufungiwa crop support
Kupandiwa
-Unakabidhiwa greenhouse/Net House ,ikiwa imekamilika
Kutembelewa na Kupewa ushauri wa mara kwa mara
Kupima Udongo

Kusaidiwa kutafuta Soko la Ndani Na Nje ya Nchi. Mfano kwa sasa tuna soko linalohitaji zaidi ya tani 3 za nyanya kila wiki. Nyanya zinazohitajika ni zile zinazopandwa kwenye greenhouse. Bado hakuna wakulima walioweza kuhudumia soko hilo
Nyongeza
-Tunatumia Materials kutoka ISRAEL, Na tuna wataalam waliobobea katika ujenzi wa greenhouse /net house Kwa muda mrefu pia wataalam wa kilimo.
Tutakufuata popote pale ulipo Tanzania Tanzania

Kwa Mawasiliano
Piga: 0763 071007
email: ushauri@kilimo.net

Response to "FURSA KUPITIA TEKNOLOJIA YA KILIMO CHA GREENHOUSE"

  • Ahsanteni sana kwa kunifungua macho, kwakweli nimehamasika sana kwa maelezo yenu pamoja na picha.
    Wacha nijipange nikiwa tayari tutawasiliana…..Inshallah..

  • Una maanisha nini unaposema Greenhouse na Nethouse? Ni kitu kimoja au ni vitu viwili tofauti? Nauliza kwa sababu hakuna popote kwenye maelezo yenu mnapolifafanua hili!

  • Habari ndugu, swali langu ni je? kilimo cha vanila kwa kutumia green house ya net je kitafaa kwa jiji la Dare es salaam? na jingine kulimo cha mipapai je kinafaa kwenye green house? napenda pia kufahamu ofisi zenu zipo wapi

  • Tunahitaji Green house yenye ukubwa wa m8xm15 zinazofaa kwenye maeneo ya joto,
    Tupo mkoa wa Shinyanga katika manispaa Shinyanga,tujulishe gharama halisinaitachukua muda gani kufungwa
    pia utaratibu wa malipo ukoje?
    Ahsante
    Jane

  • Leave a Reply to Baumba Chogero Cancel reply

    Your email address will not be published. Required fields are marked *